Na. Elinipa Lupembe.
Shirika la Maendeleo ya Kimàtaifa la nchini Denimaki (DANIDA) limeridhishwa na kupongeza utekelezaji wa mradi wa kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto, unaotekelezwa katika halmashauri ya wilaya ya Arusha, mradi unaofadhiliwa na mfuko huo, kupitia ASAS ya Foundation For Civil Society na kutekelezwa na ASAS ya Center for Women and Children Development (CWCD) ya Arusha.
Wadau hao wa maendeleo, wameridhishwa na utekelezaji wa mradi huo, mara baada ya kutembelea baadhi ya klabu za kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto, katika shule ya msingi Ilboru kitengo cha elimu maalum na klabu ya wasichana shule ya sekondari Ilkiding'a na kujionea namna watoto walivyojengewa uwezo wa kujitambua, kutambua haki na wajibu wao, kujithamini, kutambua aina za ukalitili, kupinga ukatili pamoja na kutoa taarifa pindi wapofanyiwa ukatili.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mwenyekiti wa Bodi ya shirika la Foundatio for Civil Society, Sosthenance Sambua, amethibitisha kuridhishwa na utekelzaji wa shughuli zinazofanywa na halmashauri kupitia miradi inayofadhiliwa na DANIDA kupitia FCS na kusistiza kuwa, kujionea namna watoto wa kike wanavyojiamini na uwezo wa kujitegemea kupitia mafunzo ya ujasiriamali, hali inaonyesha namna gani kazi nzuri inafanyika.
"Ujuzi mlioputa, tumieni kwa kuwaelimisha wasichana wengine shule na hata nyumbani kwenye jamii zenu, lakini nikuombe mkurugenzi kupitia Baraza la Madiwani, kuanza kuwa mipango mikakati ya kupata rasilimali za kuendeleza uwepo wa klabu za watoto shuleni, hata pale ambapo miradi ya wafadhili itafikia ukomo" amesistiza Sambua
Naye Mwenyekiti wa halmashauri ya Arusha, Mheshimiwa Ojungu Salekwa, amekiri kuwa jamii anayotokea yeye ni waathirika wakubwa wa ukatili wa wanawake na watoto unaotokana na mila na desturi za kabila lao la kimasaai, ila wao kama viongozi wa jamii, wako mstari wa mbele kupambana na ukatili huo kwa kuelimisha jamii yao, kuachana na mila hizo potofu, zinazoathiri kwa kiasi kikubwa maendeleo ya wanawake na familia kwa ujumla.
Mkurugenzi mtendaji, halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi, licha ya kuwashukuru wadau hao wa maendeleo, ameahidi kuendelea kusimamia vema utekelezaji wa miradi hiyo ili iwe endelevu kwa faida ya sasa na vizazi vijavyo na kuongeza kuwa serikali inaweka mazingira rafiki kwa wadau, kwa kuwa inathamini michango ya wadau, michango ambayo kimsingi inatekeleza malengo na mikakati ya serikali kwa manufaa ya wananchi na Taifa kwa ujumla.
"Serikali inaweka mazingira rafiki kwa wadau wa maendeleo wa ndani na nje yanchi, lengo likiwa kuwapa fursa kushirikiana na serikali kusukuma gurudumu la maendeleo, niwashukuru sana DANIDA kwa miradi ya kupinga ukatili wa kijinsia, mnayoifadhili katika halmashauri ya Arusha, miradi ambayo inaleta matoke chanya hasa kwa watoto wa kike, watoto ambao, walionekana ni wanyonge katika jamii" amesisitiza mkurugenzi Msumi.
Klabu hizo za watoto shuleni, zimeonesha mafanikio makubwa sana kwa wanafunzi wasichana, kwa kuleta mapinduzi ya kijamii na hata kitaaluma pia, wanafunzi wa kike wameweza kujifunza stadi mbalimbali za maisha, ikiwemo ujasiri wa kupinga ukatili, namna ya kukabiliana na changamoto za usichana, afya ya uzazi kwa vijana, ujasiriamali, stadi ambazo zimepunguza mimba shuleni, ndoa za utotoni, utoro shukeni na kupandisha kiwango cha taaluma kwa watoto wa kike.
Mwenyekiti wa klabu ya wasichana, shule ya sekondari ya Ilkiding'a Maurine Philip kidato cha (IV), ameweka wazi kuwa, klabu ya wasichana shuleni, imewajengea wasichana uwezo wa kuwa wajasiri katika maamuzi, katika masomo yao na kuthibitisha kuwa wasichana wengi kwa sasa wameamua kupambana kujikita kwenye masomo ya Sayansi na wa wanafanya vizuri jambo ambalo hapo awali wasichana waliogopa kusoma masoma ya Sayansi.
"Tukiwa kwenye klabu, tunafundishwa masuala ya kijamii pamoja na ujasiliamali unaotuwezesha kutengeneza taulo za kike, kwa ajili yetu na wasichana wengine wasio na uwezo, lakini pia klabu imewezesha wasichana hata wasio kwenye kalabu kuwa active katika masomo, wasichana wengi wanafanya vizuri kwenye amsomo na hata katika masomo ya Sayansi, masomo ambayo zamani wasichana wengi tulikuwa tunayaogopa sana" amesistiza mwanafunzi Maurine.
Hata hivyo, ziara hiyo ilivuta hisia kali pale walipokutana na klabu ya watoto wenye ulemavu wa kusikia kitengo maalum, shule ya msingi Ilboru, waliojengewa uwezo wa kujiamini wakifanya igizo la ukatili kwa walemavu pamoja na mabango yaliyokuwa na jumbe mbalimbali zikielezea kujiamini kwao, na jamii iwaamini kwamba wao wanafundishishika na wanauwezo wa kufanya kazi kama watu wengine.
Arusha DC KaziInaendelea✍✍
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.