• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

DAS Arumeru aagiza wananchi waliojenga kuta kuzuia maji kata za Kiranyi na Oloirieni, kubomoa mara moja.

Posted on: April 11th, 2018

Katibu Tawala wilaya ya Arumeru, Timotheo Mnzava amewaagiza wananchi wa kata za Kiranyi na Oloirien halmashauri ya Arusha, waliojgenga uzio wa kuta kwenye nyumba zao zinazozuia maji kupita, kubomoa mara moja ili kuruhusu maji kupita wakati wa mvua ili kuepusha madhara makubwa zaidi yanayoweza kutokea.    

Katibu Tawala huyo, ametoa agizo hilo kufuatia madhara waliyoyapata wakazi wa kata hizo, yaliyotokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha, karibu maeneo yote Tanzania na kuwasababishia hasara kubwa wakazi hao.    

Hata hivyo Mnzava amefikia uamuzi huo mara baada ya wananchi hao wenyewe, kumuelezea sababu za maji hayo ya mvua kuharibu mali zao, wakati alipowatembelea na kujionea madhara waliyoyapata ikiwemo kuta kuanguka na maji kujaa ndani ya nyumba zao, na kusababisha uharibifu wa thamani zote za ndani  huku wengine wakilazimika kuhama nyumba zao kwa hofu.     

Wananchi hao, wamemueleza Katibu Tawala kuwa, maji yanajaa na kuingia kwenye nyumba za watu, kutokana na ubinafsi wa kila mtu kujijengea kuta kuzunguka mipaka ya kiwanja na kusababisha maji kukosa mwelekeo na kuleta madhara hayo yaliyotokea.      

Titus Mrema mkazi wa Kirayi amesema kuwa, pindi mvua kubwa zinaponyesha, maji hukosa mahali pa kupita kutokana na kuta zilizojengwa na badala yake hujaa ndani ya nyumba za watu na kusababisha madha haya mnayoyaona.     

Wananchi hao walimtembeza katibu Tawala na kushuhudia namna uzio wa kuta zilivyojengwa na kuzuia maji kupita,  jambo lililosababisha baadhi ya kuta kuanguka na nyingine kutobolewa kwa dharura ili kuruhusu maji kupita.    

Baadhi ya wananchi wamesema kuwa chanzo cha maji hayo kukosa uelekeo ni kubomolewa kwa tuta lilolopo katika eneo la Kiyoga, lililokuwa limejengwa na wazee miaka ya nyuma, kwa lengo la kupunguza kasi ya maji na maji hayo kuelekezwa mtoni.

Samwel Ngarabali mkazi wa Ilkiding'a na diwani mstaafu amemthibitishia Katibu Tawala kuwa, jambo la msingi ni kudhibiti maji eneo la Kiyoga na Olturoto,ambapo hapo awali kulikuwa na tuta linalozuia maji na kuelekeza maji hayo mtoni, lakini kuna watu wamebomoa tuta hilo kuepusha maji kupita kwenye mashamba yao, jambo linalosababisha madhara kwa wakazi waishio maeneo mengi ya kanda za chini.      

Hata hivyo Mnzava ameunda timu ya watalamu kuchunguza zaidi  na kuthibitisha ukweli juu ya tuta hilo, eneo la Kiyoga na kutafuta namna ya kudhibiti maji hayo katika eneo hilo.     

Naye Hussein Hudison, mkazi wa Ilkiurei ameunga mkono agizo hilo la Katibu Tawala, na kusema kuwa inawabidi wakakae mkutano wa kitongoji na kukubaliana kwenda kubomoa kuta hizo kwani watu wote wanafahamika, na kukaa na kukubaliana na watu hao ikishindikana, wananchi kwa pamoja kuamua kufanya maamuzi magumu.      

Hussein Hudison mkazi wa Ilkiurei ameunga mkono agizo hilo na kusema kuwa inawabidi wakakae mkutano wa kitongoji na kukubaliana kwenda kubomoa kuta ambazo zinasabanpbisha madhara hayo, kwani watu wote waliojenga kuta zinazozuia maji zinafahamika, na kukaa na kukubaliana na watu hao ikishindikana, wananchi kwa pamoja kuamua kufanya maamuzi magumu.     

Mpaka inaandikwa habari hii, bado haijafahamika thamani halisi ya hasara ya mali za wananchi iliyopatikana kutokana na mvua hizo, thamani halisi itatolewa baada ya watalamu kukamilisha tathmini hiyo.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.