Mkuu mteule wa wilaya ya Arumeru Mhe. Emmanuela Kaganda Mtaifikolo ameapishwa mapema leo na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongela kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa mkao wa Arusha.
Mheshimiwa Emmanuela amekula kiapo hicho kwa mujibu wa sheria, tayari kwa kwenda kuwahudumia wananchi wa halmashauri mbili za Arusha na Meru.
Katika hafla hiyo jumla ya wakuu wa wilaya wanne wameapishwa ikiwemo mkuu wa wilaya ya Arusha, Longido, Mkuu wa ya Monduli pamoja na mkuu wa wilaya ya Arumeru.
Awali Wananchi wa halmashauri ya Arusha, wanakukaribish na kukutakia kila la kheri katika kutekeleza majukumu yako mapya ya kuwahudumia wananchi.
ARUSHA DC Yetu, Tushirikiane kuijenga"
KaziInaendelea✍✍
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.