• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

DC ARUMERU AKABIDHIWA MADARASA YA MPANGO WA MAPAMBANO YA UVIKO 19, SEKONDARI MATEVESI

Posted on: December 8th, 2021

Na. Elinipa Lupembe.

Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mhandisi Richard Ruyango, amekabidhiwa rasmi jengo la vyumba vitatu vya madarasa, meza na viti 150, vyenye thamani ya shilingi milioni 60, katika shule ya sekondari Mateves, halmashauri ya Arusha, mara baada ya kukamilika kwa ujenzi huo, kufuatia agizo la mheshimiwa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan,  kukamilisha ujenzi huo ifikapo tarehe 15.12.2021.

Akipokea jengo hilo, mkuu huyo wa wilaya, amewapongeza wasimamizi na watekelezaji wote wa mradi huo, kuanzia ngazi ya halmashauri, kata, shule kamati ya ujenzi pamoja na mafundi wazalendo, kwa kuwezesha kukamilisha ujenzi huo kwa wakati na zaidi jengo hilo likiwa kwenye viwango vya ubora, vinavyoakisi thamani ya pesa zilizotumika.

Mhandisi Ruyango amekwenda mbali zaidi kwa kuishukuru Serikali ya awamu ya sita, inayoongozwa na mheshimiwa Rais, mama Samia Suluhu, kwa kuboresha miundombinu ya shule, licha ya kuwa na mazingira bora ya kujifunzia na kufundishia, kubwa zaidi utekelezaji wa mpango wa mapambano dhidi ya UVIKO 19, kwa walimu na wanafunzi wawapo darasani.

"Shilingi bilioni 2 tulizopokea za ni fedha nyingi sana, tusingeweza kuzipata kwa kuchangisha kwa wananchi, ninamshukuru na kumpongeza sana Rais wetu, amefanya mapinduzi makubwa sana katika sekta ya Elimu kwa muda mfupi, haijawahi kutokea, watoto wetu watasoma kwa raha lakini na wananchi nao wamepunguziwa mzigo wa michango ya ujenzi wa madarasa mwaka huu" amesisitiza Mkuu huyo wa wilaya.

Naye mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi, ameweka wazi kuwa, halmashauri inaendelea na ukamilishaji wa ujenzi wa vyumba 100 vya madarasa na samani zake, ikiwa ni madarasa 96 kwa shule 30 za sekondari na madarasa 4 kwa shule  2 za msingi shikizi, huku baadhi ya madarasa yakiwa tayari yamekamilika, na maendeleo ya mradi mzima ukiwa umefikia  zaidi ya 90% za ukamilishaji.

Hata hivyo, Makamu Mwenyekiti halmasahuri ya Arusha na Diwani wa kata ya Mateves, ambapo ujenzi katika shule ya kata yake umekamilika na kukabidhiwa, Mhe. Freddy Mollel, licha ya kuipongeza serikali, ameweka wazi kuwa, wananchi wamepata matumaini makubwa sana na serikali yao, kwa kuwa wana uhakika watoto wao waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza Januari 2022, wataanza masomo yao kwa wakati, huku wakishukuru kwa kupumzishwa na michango ya ujenzi wa madarasa kwa mwaka huu.

"Niseme tuu, tunaendelea kuishukuru na kuipongeza serikali ya awamu ya sita, kwa kutujengea madarasa ya kidato cha kwanza, kwa idadi ya wanafaunzi 300, waliopangiwa shuleni hapa, kama si fedha hizi, tungekuwa na hali ngumu sana, kiukweli wananchi wamepumzika na michango, michango ambayo ilikuwa ni mzigo kwao katika maeneo mengi"amefafanua Makamu huyo Mwenyekiti.

Awali, Mkuu wa shule ya sekondari, Mateves, Mwalimu Sayuni Tarimo, ameishukuru serikali kwa kuwapatia idadi hiyo ya madarasa, na kuahidi kuwasimamia wanafunzi kuyatunza madarasa hayo pamoja na samani zake kwa ajili ya sasa na vizazi vijavyo huku wakifundisha kwa bidii na kupandisha kiwango cha taaluma sambamba na mapambano dhidi ya UVIKO 19.


ARUSHA DC

KaziInaendelea✍✍












Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.