Na Elinipa Lupembe
Mkuu wa wilaya ya Arumeru, Mhe. Emmanuela Mtatifikolo Kaganda akikagua hali ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi kituo kipya cha Afya kata ya Bwawani mradi unaotekelzwa na serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF kwa gharama ya shilingi milioni 357.
Mkuu huyo wa wilaya ametumia nafasi hiyo kuishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za mradi huo muhimu kwa wananchi ukiwa na lengo la kusogeza huduma za afya karibu na wananchi husasani waishi vijijini.
"Kwa niaba ya wananchi wa Bwawani, ninaiponheza na kuishukru serikali ya mama Samia kwa kusogeza huduma kwa wananchi ambao waliteseka kuwenda mbali kupata hudumazp za afya huku kina mama wajawazito na watoto wakipoteza maisha kutokana na kukosa ama kuchelewa kupata huduma za afya, uwepo wa kituo cha afya Bwawani utapunguza na kuondoa vifo visisvyo vya lazima vya kinamama na watoto" Amesisitiza Mhe. Emmanuela
Katika ziara hiyo Mhe. Emmanuela amewataka watalamu halmashauri ya Arusha kusimamia mradi huo muhimu kwa wananchi wa Bwawani na kuhakikisha unakamilika kwa wakati kulingana na muda wa mkataba ukiwa na viwango vya ubora unaolingana na thamani ya fedha zilizotolewa na serikali.
Mradi huo wa ujenzi wa kituo cha afya unategemea kukamilia mwishoni mwa mwezi Oktoba, 2023 na unajumuisha ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD), ujenzi wa wodi ya mama na mtoto ( maternitu ward) pamoja na nyumba ya watumsihi yenye kuisshi familia tatu (3 in 1).
ARUSHA DC ni Yetu, Tushirikiane Kuijenga"
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.