Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mhe. Emanuela Mtatifikolo Kaganda pamoja na Mwenyekiti wa CCM wilaya yaArumeru, wameongoza mchango mdogo kwa ajili ya kuoata maziwa ya mtoto kwa familia ya Samson Silamoi ambao nyumba yao umechukuliwa na maji kutokana na mvua kubwa iliyonysha usiku wa tarehe 23.Machi halmashauri ya Arusha.
Baada ya familia hiyo yenye mtoto mmoja mdogo, kueleza nyumba yao kuchukuliwa na maji na kuwa wanaishi kwa jirani, viongozi hao wa Chama na Serikali walipitisha mchango na kwa watu waliombatana nao na kufanikiwa kupata shilingi laki 2 zikiwa ni gedha kwa ajili ya kupata chakula pamoja na maziwa ya mtoto.
Hata hivyo Mheshimiwa Mkuu wa wilaya amewashukuru wananachi kwa kuisaidia hifadhi kaya hiyo na kuwawapa misaada mbalimbali ya kibinadamu na kusisitiza udugu huo uendelee kuwepo katika maisha ya kila siku ya wanaarumeru.
"Ninashukuru kwa kuwa wananchi wote waliungana kukabiliana na majanga yaliyotokea kwa kuwasaidia wale walioathithika zaidi, huu ndio upendo ambao Mwenyenzi Mungu ameusisitiza katika maisha yetu wanadamu". Amesisitiza Mhe. Emanuela
Akizungumza wakati akikabidhi kiasi hicho cha fedha kwa familia ya Samson, Mwenyekiti wa CCM Arumeru, Noah Severe ametoa pole kwa familia hiyo na kuwataka kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu na kuwatia moyo kiwa matatizo ni sehemu ya maisha ya binadamu.
"Poleni sana kwa yaliyotokea mnapaswa kushukuru kwa yote, sisi kama viongozi wa Chama na Serikali, hatutawacha tutakuwa pamoja na kuhakikisha mnarejea kwenye amisha yenu ya kawaida".Amesisitiza Mwenyekiti Severe.
Katika ziara hiyo Mkuu wa Wilaya ya Arumeru aliambatana na Kamati ya ulinzi na Usalama pamoja na viongozi wa CCM wilaya ya Arumeru.
ARUMERU
#kaziinaendela✍✍✍
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.