Na Elinipa Lupembe
#Waheshimiwa Madiwani mnalo jukumu la kusimamia hali ya chakula katika maeneo yetu, tumepita kwenye ukame, lakini tuko kwenye kipindi cha mavuno, simamieni wqnanchi wenu kutunza vizuri mazao ya chakula, hususani kwenye maeneo ambayo mazao ya chakula yamepatikana.
#Simamieni shughuli zote za utekelezaji wa maendeleo kwenye kata zenu, tumieni muda kutatua migogoro na changamoto zinazowakabili wananchi, wananchi wana kero nyingi na wanajaa kwenye ofisi ya Mkuu ya wilaya, mkizishughulikiwa vizuri na kwa haki, wananchi wataendelea kuiamini serikali yao
#Wasimamieni Watendaji na Wenyeviti wa Vijiji ili kufanyae mikutano ya kisheria ya kila robo ya mwaka, simamieni usomaji wa Taarifa za Mapato na Matumizi, ili wananchi wafahamu maendeleo ya vijiji vyao, Kamati ya Usalama ilitoa maelekezo Kila kijiji wa hakikishe mpaka mwezi wa Julai, wakamilishe mikutano ya usomaji na mapato na matumizi na taarifa ziwasilishwe kwenye ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji.
#Ameweka wazi kuwa Wilaya ya Arumeru ni lango la Jiji, tume barikiwa kupata wageni wengi wanaopita kwenye wilaya yetu, Mazingira yetu ni machafu, Simamieni usafishaji wa mazingi, na kurudisha rasmi utaratibu wa kufanya usagi wa jumla kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi, Kiengo cha Usafi tozeni faini kwa watu wanaochafua mazingira, Kila halmashauri itengeneze 'Kikosi kazi kwa ajili ya suala la usafi, na faini za elfu hamsini zita rudi kwa wanao tupa taka hivyo.
#Simamieni suala zima la ulinzi na Usalama wa wananchi na mali zao, kumekuwa na tabia za ubakaji,ulevi na uuzaji wa pombe haramu, matumizi ya bangi ni changamoto katika maeneo yetu, Mkiwa kama viongozi simamieni na kupambana na wahalifu ikiwezekana toeni taarifa za siri za wahalifu kwa kushirikiana na jeshi la polisi, kwa kufanya hivi wananchi watakuwa salama.
#Tendelee kusimamia ukusanyaji wa mapato na kubuni vyanzo vipya vya mapato pamoja na kuhoji matumizi ya mapato hayo na jinsi ambavyo fedha hizo zina patikana.
#Simamieni utekelzaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwenye kata zetu tuichukulie uzito unaostahili kwani Mhe. Raisi Samia Suluhu Hassani, na serikali yake yote ya awamu ya sita Wana fanya kazi kubwa sana ya kuleta fedha nyingi sana kwenye maeneo yetu.
ARUSHA DC NI YETU, TUSHIRIKIANE KUIJENGA
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.