Na Elinipa Lupembe
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Emmanuela Mtatifikolo Kaganda amewatembelea na kuwajulia hali majeruhi wa ajali ya gari kwaaliolazwa kwenye hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Arusha Mount Meru, iliyotokea tarehe 14.09.2023, eneo la Kisongo mkoani Arusha, iliyohuaisha gari aina ya Toyota Hiace.
Mhe. Emmanuela amefika hospitalini hapo ili kuwajulia hali majeruhi wa ajali pamoja na kuwapa pole ndugu jamaa na marafiki waliopoteza ndugu zao walifariki kwenye ajali hiyo, waliofika kwenye jengo la kuhifadhia maiti, kubeba miili ya wapendwa wao.
Aidha, amesema kuwa, Serikali imefanya juhudi kubwa katika suala la uokoaji wa maisha ya watanzania hao kupitia jeshi la polisi tangu ajali ilipotokea na kuhakikisha afya za majeruhi wote zinaimarika bila kuwadai gharama zozote za matibabu hadi pale watakapo pata nafuu na kuendelea na majukumu yao ya ujenzi wa Taifa.
"Serikali imechukua jukumu la kugharamia gharama zote za matibabu kwa majeruhi wa ajali hiyo hadi pale afya zao zitakapoimarika na kurejea kwenye majukumu yao ya kawaida" Amesema.
Hata hivyo ametoa wito kwa madereva wote wa magari kuwa waangalifu wanapotumia vyombo vya moto kwa kuzingatia sheria zote za barabarani ili kuepusha ajali zisizo za lazima, zinazotokea mara kwa mara na kugharimu maisha ya watanzania.
Naye Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha Mount Meru, Dkt. Alex Erinest amesema kuwa walipokea miili 6 na majeruhi 9, ambapo miili 5 imetambuliwa na ndugu zao na mwili mmoja bado haujatambulika.
Aidha, majeruhi 7 wamelazwa kwenye wodi huku majeruhi 2 wakiwa wamelazwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi huku hali zao zikiendelea kuimarika kutokana na juhudi zinazoendelea kufanywa na jopo la madaktari wakishirikiana na wauguzi.
Hata hivyo ametoa wito kwa wananchi ambao ndugu yao haonekani, kufika hospitalini hapo kwaajili ya kupata taarifa na kuutambua mwili huo ambao hadi sasa haujatambulika.
MATUKIO KATIKA PICHA
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.