Na. Elinipa Lupembe.
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mhandisi Richard Ruyango, amewataka walimu kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya UVIKO 19 kwa, kufuata maelekezo yanayotolewa na wahudumu wa afya na zaidi kujitokeza kupata chanjo ya ugonjwa huo, ugonjwa ambao unahatarisha maisha na kuua watu wengi duniani, huku kukiwa tayari kumeibuka aina nyingine ya kirusi kinachofahamika kwa jina la 'Omicrone'.
Mkuu huyo wa wilaya ametoa rai hiyo, kwa walimu wa shule ya sekondari Ilkiding'a mara baada kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa vyumba 11 vya madarasa shuleni hapo, madarasa yanayojengwa kupitia fedha za mpango wa ustawi wa Taifa wa mapambano dhidi ya UVIKO 19, na kupata wasaa wa kuzungumza na walimu hao, masuala mbalimbali ya miundo mbinu ya shule pamoja na hali halisi ya utumishi wa Umma.
Mhandisi Ruyango, ameweka wazi kuwa, lengo la serikali kujenga miundo mbinu ya madarasa nchini kote, ni kupunguza msongamano wa wanafunzi madarasani, ikiwa ni mpango wa Taifa wa kupambana na UVIKO 19, kwa walimu na wanafunzi wakati wa kufundisha na kujifunza.
Serikali imeshatimiza wajibu wake, kwa kuweka mazingira bora ya kujifunzia na kufundishia, kazi iliyobaki ni walimu kuwaongoza wanafunzi katika matumizi sahihi ya miundo mbinu hiyo, ikiwemo kuyatunza madarasa hayo na zaidi kiwasimamia kupambana na UVIKO 19, jukumu ambalo lipo mikononi mwa walimu wote ambao ni walezi wa wanafunzi wawapo shuleni.
Aidha amewasisitiza walimu hao, licha ya kuendelea kujikinga na UVIKO 19, mapambano hayo yanakwenda sambamba na uchanjaji, Serikli imeleta chanjo awamu ya kwanza na ya pili, huku walimu wakiwa kwenye kundi lililopewa kipaumbele, na kuongeza kuwa walimu watumie fursa hiyo kuchanja huku wakiwaelimisha wanafunzi wanao wasimamia kuchanja pia.
"Jamii inawaaamini sana walimu, tumieni fursa hiyo kuokoa maisha ya watu wengi zaidi, kwa kuwaelemisha watu kufahamu umuhimu wa kupata chanjo ya UVIKO 19, pamoja na ninyi kuwa mfano wa kuchanja" amesisitiza Mkuu huyo wa Wilaya.
Hata hivyo walimu hao, wa shule ya sekondari Ilkiding'a,wameishukuru serikali ya awamu ya sita, inayoongozwa na mheshimwa Rais Mama Samia Suluhu, kwa kujenga vyumba 11 vya madarasa kwa wakati mmoja shuleni hapo, jambo ambalo wamekiri halijawahi kutokea shuleni hapo ama shule za jirani na kuthibitisha kuwa madarasa hayo yatapunguza msongamano madarasani kulingana na idadi kubwa ya wanafunzi shuleni hapo.
Aidha walimu hao wamemuahidi mkuu wao wa wilaya, kwenda kuchanaja kwa wale ambao hawajachanja na kuendelea kuelimisha jamii katika maeneo yao, juu ya umuhimu wa chanjo ya UVIKO 19, ugonjwa ambao licha ya kupoteza maisha ya watu wengi lakini pia unaondoa amani katika jamii kwa kuwa na wasiwasi mkubwa.
Hata hivyo mkuu huyo wa wilaya amewataka wananchi wote kuchukua tahadhari dhidi ya UVIKO 19, kwa kubwa bado ni tishio kwa dunia kutokana na kirusi hicho kuwa na tabia ya kujibadilisha, amewasisititiaz wanachi wote kunawa mikono kwa sabuni maji tirirka, kuepuka msongamano, kutumia vitakasa mikono kuvaa barakoa zaidi ya yote kupata chanjo, chanjo ambayo inapunguza makali ya virusi hao pindi mtu atakapougua mardhi hayo.
ARUSHA DC
#KaziInaendelee✍✍✍
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.