• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

DC ARUMERU AWATAKA WATENDAJI KUHAKIKISHA ZOEZI LA SENSA LINAFANIKIWA KAMA LILIVYOPANGWA

Posted on: August 17th, 2022


Na Elinipa Lupembe.

Mwenyekiti wa kamati ya Sensa wilaya na Mkuu wa wilaya ya Arumeru, na Mhandisi Richard Ruyango, amewataka watendaji wa halmashauri ya Arusha, kushiriki kwa pamoja kuhakikisha wananchi wa halmashauri hiyo wanahesabiwa siki ya Sensa ya watu na makazi 23.08.2022 .

Mkuu huyo wa wilaya ameyasema hayo, wakati wa kikao kazi cha Sensa , kilichowakutanisha Wakuu wa Idara na Vitengo, Maafisa Tarafa, Watendaji wa Kata na Vijiji pamoja wa halmashauri hiyo, kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya Arusha.

Hata hivyo Mhandisi Ruyango amewataka Maafisa hao kushirikiana na viongozi wote wa vyama na serikali,  dini, mila na viongozi wa jumuia mbalimbali ndani ya wilaya ya Arumeru, katika maeneo yao kuhakikisha wanashiriki zoezi hili la Sensa ya watu na makazi kwa kuhamasisha watu wanaowaongoaza katika maeneo yao kuhesabiwa katika zoezi hilo la Sensa.

Aidha amezitaka kamati za Sensa za kata na vijiji kujikita katika kutoa taarifa zote za kijamii, zitakazohitajika kwenye dododso la Jamii kuwa wana uelewa wa kutosha wa eneo hilo pamoja na huduma zinazopatikana katika maeneo yao.

"Makarani wanapofanya kazi kwenye maeneo yetu, viongozi wote tuhakikishe taarifa zote za huduma za kijamii zinaingizwa kwenye dodoso la jamii  ikiwemo  taasisi zilizopo katika eneo yako, miundombinu ya majinna barabara, matukio mbalimbali kama majanga ya moto na njaa, hii inawahusu moja kwa moja viongozi" Amesisitiza Mkuu huyo wa wilaya

Akizungumza kwa niaba ya waheshimiwa madiwani, Mwenyekiti wa halmashauri ya Arusha, Mhe. Ojung'u Salekwa amebainisha kuwa tayayari wenyeviti wa Sensa ngazi ya kata ambao ni madiwani, wameanza kuhamasisha wananchi kushiriki zoezi hilo la Sensa katika maeneo yao na kuweka wazi kuwa wananchi wengi wana uelewa juu ya Sensa ya mwaka huu kutokana na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan  kuifanya kuwa shirikishi kwa kutumia majukwaa tofauti kuielezea Sensa.

Naye Mkurugenzi Mtendaji, halmasahuri ya Arusha, Seleman Msumi amesema kuwa yeye na watalamu wa halmashauri hiyo wamejipanga kuhakikisha zoezi la Sensa linafanyika kwa usahihi kwa kuhamasisha pamoja na kuhakikisha kila mkazi wa halmasahuri hiyo anahesabiwa na kama ilivyo malengo ya serikali.

Awali mkuu wa wilaya ya Arumeru, atakutana na viongozi wote wa wananchi na kijamii  kimakundi ikiwemo, viongozi wa vyama vya siasa, viongozi wa mila na dini.


SHIRIKI SENSA YA WATU NA MAKAZI

JIANDAE KUHESABIWA 23.08.2022.















Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.