HAYAWI HAYAWI YAMEKUWA
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mhandisi Richard Ruyango, anawatangazia wananchi wote, kuhudhuria halfa fupi ya kukabidhi mikopo kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu, itakayofanyika siku ya Jumatatu tarehe 01.11.2021 kuanzia saa 03:00 asubuhi, Kwenye Ukumbi wa mikutano halmashauri ya Arusha.
Jumla ya shilingi milioni 384 zitakabidhiwa kwa Vikundi 50 vya wanawake na Vijana na Watu 2 wenye Ulemavu, ikiwa ni fedha za asilimia 10 ya Mapato ya ndani ya halmashauri ya Arusha kwa kipindi cha robo ya kwanza kwa mwaka wa fedha 2021/2022 cha kuanzi mwezi Julai hadi Septemba 2021.
NYOTE MNAKARIBISHWA!!
ARUSHA DC
#KaziIendelee
#kaziinaendelea
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.