• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

DC Kimanta awaaga watumishi wa Arusha DC kwa kuwamwagia sifa lukuki

Posted on: August 2nd, 2018

Na. Elinipa Lupembe

Mkuu wa wilaya ya Monduli , mheshimiwa Idd Kimanta amehitimisha kazi ya kukaimu ukuu wa wilaya ya Arumeru jana, kwa kumtambulisha na kumka mkuu mpya wa wilaya ya Arumeru.

Mheshimiwa Kimanta amemtambulisha mkuu wa wilaya ya Arumeru, mheshimiwa Jerry Muro kwa watumishi wa wilaya hiyo yenye halmashauri  mbili za Meru na Arusha.

Akizungumza wakati wa utambulisho huo,  Mheshimiwa Kimanta ameanza kwa kumpongeza  Jerry Muro kwa kuteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Arumeru, na kumtaka kuitumikia nafasi hiyo kwa uadilifu kama Rais alivyomuamini.

Mhe. Kimanta amefafanua kuwa, hana mashaka na uteuzi wa mheshimiwa rais kwa kuwa kila mkuu wa wilaya, anayemteua anauzoefu na kazi ya kuwahudumia wananchi.

 "Kwa taaluma ya Jerry Muro, sina mashaka na uchapa kazi wake, na uwezo wake wa kuwahudumia wananchi wanyonge, hivyo mheshimiwa rais hakubahatisha kumteua" amesema mheshimiwa Kimanta.

Hata hivyo amewataka watumishi wa halmashauri ya Arusha, kumpa ushirikiano kama waliompa yeye katika kipindi chote alichofanya kazi katika halmashauri hiyo.

Mheshimiwa Kimanta amekiri,  kuridhishwa na uwezo wa watumishi wa halmashauri ya Arusha na hakusita kuwapongeza watumishi hao mbele ya mkuu huyo mpya wa wilaya ya Arumeru.

" Mheshimiwa mkuu wa wilaya ya Arumeru, ninakukabidhi watumishi hawa, wakiwa weupe kama kitambaa, wakiwa wenye afya njema, wenye nyuso za bashasha na uwezo mkubwa wa kufanyakazi kwa weledi huku wakitekeleza Ilani ya Chama Tawala,  chama cha Mapinduzi CCM" amesema  mheshimiwa Kimanta.  

Ameongeza kuwa, kwa kipindi kifupi alichofanyakazi wilaya ya Arumeru,  amekiri kuona utendaji uliotukuka wa watumishi wa halmashauri ya Arusha wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Dkt. Wilson Mahera, watumishi waliojikita zaidi kwenye kazi za kuwahudumia wananchi na si kwenye migogoro na ugomvi baina ya watumishi wenyewe.

Amekiri kuwa, watumishi wanafanyakazi wakiwa na amani ya kazi, kwa kuwa hajawahi kupokea lalamiko la mtumishi yoyote, akimlalamikia mtumishi mwenzake, jambo lililomuwezesha kujikita kwenye kufanyakazi zaidi na sio kusuluhisha kesi za ugomvi baina ya watumishi, na kukiri kuwa, hali hiyo ni tofauti sana na maeneo mengine aliyowahi kufanyakazi.

Mkuu wa wilaya ya Monduli Idd Kimanta amekaimu kuitimikia wilaya ya Arumeru kwa takribani miezi nane sasa tangu aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Arumeru kuteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Manyara, mheshimiwa Pastory Mnyeti mapema mwishoni mwa mwaka 2017.

Licha ya ukubwa wa wilaya ya Arumeru kwa kuwa,  na halmashauri mbili ya Arusha na Meru, amefanikiwa kusimamia vema na kwa weledi  mkubwa licha ya kuzitumikia halmashauri tatu kwa wakati mmoja, kwa takribani miezi nane.  

Watumishi wa halmashauri ya Arusha, wamempongeza mkuu huyo wa wilaya ya Monduli na kuthibitisha kuwa wamefanikiwa, kujifunza mambo mengi kutokana na hekima na busara za mzee Kimanta.  

Wamesema kuwa uzoefu, busara na hekima za mkuu wa wilaya Kimanta, ni hazina kwa watumishi wa halmashauri ya Arusha na kuahidi kutumia  katika kuwatumikia wananchi.

Naye Afisa Mipango, halmashauri ya Arusha, Anastanzia Tutuba amesema kuwa amejifunza, unyenyekevu, kujishusha kwa mtu yoyote bila kujali hadhi yake pamoja na kutumia muda usikiliza zaidi.

" Mzee Kimanta ni kiongozi mbobezi mwenye tofauti, licha ya kuwa na umri mkubwa na cheo kikubwa,  lakini ni bado mnyenyekevu, anayejishusha, mwenye kusikiliza kabla ya kufanya maamuzi, kifupi ni kiongozi aliyetukuka" amesema Afisa Mipango huyo.

Matangazo

  • TANGAZO LA KAZI ZA MKATABA HALMASHAURI YA WILAYA YA ARUSHA August 14, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • KUFUATILIA NA USAMIZI WA HAKI ZA MTOTO KATIKA JAMII NI JAMBO MUHIMU

    August 25, 2025
  • RAIS SAMIA AMUAPISHA AMOS MAKALLA KUWA MKUU WA MKOA WA ARUSHA

    August 26, 2025
  • DKT. JAHANNES LEMBULUNG' LUKUMAY ACHUKUWA FOMU YA UGOMBEA UBUNGE WA CCM JIMBO LA ARUMERU MAGHARIBI

    August 25, 2025
  • KIKAO KAZI CHA WENYEVYITI WA BODI NA WATENDAJI WAKUU WA TAASISI ZA UMMA (CEOs Forum 2025)

    August 24, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.