Na Elinipa Lupembe
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Arusha ndugu Seleman Msumi, amemewapongeza wakuu wa shule za sekondari kufanya kazi kwa weledi, jambo linalosababisha halmashauri hiyo kupanda kwa kiwango cha taaluma na kuwa kinara katika matokeo ya mitihani ya Taifa kuanzia mkoa hadi Taifa.
Mkurugenzi Msumi amesema hayo wakati akifungua kikao cha wakuu wa shule za sekondari Tanzania - TAHOSSA, kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa chama cha walimu (CWT) mkoa wa Arusha kwa kuwashukuru kwa kufanya vizuri kwa vitendo katika nyaja ya kitaaluma, michezo na usimamizi wa miradi.
“Nitumie nafasi hii, kuwapongeza kwa matokeo mazuri ya kidato cha nne, na hasa yale ya kidato cha sita, tumefanikiwa kuendelea kuondoa alama sifuri ni matarajio yetu kuondoa zero kabisa na kuoandisha ufaulu zaidi niwasiistize suala la uadilifu hasa katika usimamizi wa mitihani kwa kuz
Akiwasilisha taarifa ya mwaka, mwenyekiti wa TAHOSSA halmashauri ya Arusha, Mwl.Sunday Joseph, amesema kuwa lengo la kikao hicho ni kujadili mbinu na mikakati ya kuwaandaa wanafunzi wa kidato cha pilina cha nne kwa ajili ya mitihani ya Taifa.
Aidha amefafanua kuwa licha ya mafanikio makubwa ya chama hicho, amezitaja baadhi ya changamoto ni upatikanaji wa chakula cha mchana kwa wanafunzi unaosababishwa na baadhi ya wazazi kukaidi na wengine kushindwa kuchangia chakula na kusababisha baadhi ya watoto kushinda njaa wakati wa masomo.
“Suala la chakula bado ni changamoto na linakwamisha taaluma huku wanafunzi wakishindwa kufanya vizuri katika masomo yao huku baadhi ya shule zikiwa na hazina mabweni na kufanya watoto kutembea umbali mrefu kwenda na kurudi shuleni huku wakikosa muda wa kutosha kujisomea" Amesema Mwl.Joseph
Aidha ameyataja mafanikio ya TAHOSSA ni pamoja na kupandisha kiwango cha taaluma na kuongeza ufaulu kwa shule za sekondari kwa mitihani ya Taifa na kushika nafasi za juu kimkoa na kitaifa kwa kila mwaka.
TAHOSSA wameipongeza Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mh.Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi za ujenzi na uboreshaji wa miundo mbinu, licha ya kuondoa msongamano wa wanafunzi madarasani, imerahisisha tendo la kujifunza na kufundisha na kuwafanya walimu kuwafikia wanafunzi kwa urahisi.
Naye Mkuu wa shule ya sekondari Osiligi, Mwl. Rosemary Antony amesema kuwa kikao hicho ni muhimu kwao, kinawapa fursa ya kubadilishana uzoefu na kujengeana uwezo katika nyanja mbalimbali hasa ya kitaaluma, na kuongeza kuwa siri ya mafanikio ni ushirikiano mkubwa kwa shule za kwa kufanya mitihani ya ndani ya ushindani kwa shule zote.
Awali mkutano wa TAHOSSA ngazi ya halmashauri hufanyika kwa mwaka mara mbili na huu ni mkutano wa mwisho kwa mwaka.
Arusha DC Ni yetu, Tushirikiane Kuijenga
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.