Mkurungenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi na familia yake, tayari ametimiza wajibu wake, kama mkuu wa kaya, kwa kuhesabiwa kwenye Sensa ya Watu na Makazi nyumbani kwake eneo la Sekei kijiji cha Mbalakai Kata ya Kiutu.
Mkurugenzi Msumi, amewataka wananchi wote wa halmashauri hiyo kutoa ushirikiano kwa Makarani wa Sensa watakaofika kwenye kaya zao kuhesabu huku wakitoa taarifa sahihi zitakazo hitajika kwenye dodoso la Sensa.
"Utoaji wa taarifa sahihi kwa makarani wa Sensa, itawezehsa kupata Takwimu sahihi, takwimu ambazo serikali itazitumia kupanga mipango bora ya maendeleo nchini".Amesisitiza Mkurugenzi Msumu
Aidha amewataka wakazi wa halmashauri hiyo, kufahamu kuwa zoezi la Sensa si la siku moja, hivyo endapo Karani wa Sensa hatafika kwenye kaya yako leo atafika siku inayofuata kwa kuwa zoezi linaendelea.
Zoezi la Sensa ya watu na Makazi linaendelea katika halmashauri ya Arusha,huku kukiwa na hali ya amani na utulivu, wakazi wa halmasahuri hiyo wakiwa nyumbani kusubiri Makarani wa Sensa kufika kwenye kaya zao.
HAKIKISHA UMEHESABIWA✍✍
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.