Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha amekabidhi gari lenye namba za usajili SM 9277 kwa uongozi wa shule ya sekondari Einoth, maalum kwa ajili ya matumizi ya shule hiyo.
Akizungumza wakati wa kukabidhi gari hili lwa Mwenyekiti wa Bodi ya shule, tukio lililofanyika kwenye viwanja vya makao makuu ya halmashauri ya Arusha, Mkurugenzi Mtendaji Seleman Msumi amesema kuwa, ni utaratibu wa halmashauri hiyo,kunaootokea uwepo wa gari, huzigawa kwa shule kubwa za sekondari hususani zile za bweni ili kutatua changamoto za usafiri shuleni.
Amewataka viongozi hao wa shule, kata na kijiji kuhakikisha utunzaji wa gari hilo pamoja na kuzingatia matumizi sahihi yaliyokusudiwa ambayo ni kutoa huduma ya usafiri kwa ajili shughuli za shule kwa walimu, wanafunzi na watalamu wasio walimu shuleni hapo.
Hata hivyo halmashauri ya Arusha, imetekeleza agizo la Mheshimiwa Waziri mkuu kwa halmashauri kuzipa gari shule za bweni ili kutoa huduma za usafiri shuleni
Mwenyekiti wa Bodi ya Shule Saitabau Namoyo, licha ya kuushukuru uongozi wa halmashauri hiyo kwa kuwapa gari ameweka wazi kuwa gari hilo kitendea kazi muhimu kwa shule yao na limekuja wakati muafa ili kuwahudumia walimu na wanafunzi hasa wale wa bweni pindi inapotokea dharura wakati wa usiku.
"Tulikuwa na uhitaji mkubwa sana wa gari, kutokana na shule kulazimika kuingia gharama kubwa kukodi gari pindi inaootokea kuna dharura kwa wanafunzi hasa nyakati za usiku, kuwepo kwa gari hili naamini licha ya kupunguza gharama litasaidia kuhudumia wanafunzi kwa uhuru na amani" Ameweka wazi Namoyo.
Hata hivyo mwenyekiti huyo, ameahidi kuhamasisha wazazi kununua gari aina ya 'costa' shuleni hapo kwa ajili ya walimu na wanafunzi wakati wa ziara za kimasomo
Naye Mkuu wa shule ya sekondari Einoth ameshukuru kwa kupatiwa gari na kukiri kuwa gari hilo kitendea kazi muhimu kwa shule hiyo kwa kuwa itawaondolea dhahama waliyokuwa nayo ya kukodi gari kwa ajili ya shuguli za shule jambo ambalo liliwaingiza kwenye gharama kubwa.
ARUSHA DC NI YETU, TUSHIRIKIANE KUIJENGA
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.