Elinipa Lupembe.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Arusha Seleman Msumi, amemkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Meru, Mwl. Zainabu Makwinya eneo la Peace Point Ambureni, zote zikiwa ni halmashauri za wilaya ya Arumeru.
Mkurugenzi Msumi ameukabidhi Mwenge wa Uhuru mara baada ya kukimbizwa umbali wa Kilomita 90.4 katika halmasahuri hiyo na kupitia jumla ya miradi 9 yenye thamani ya shilingi bilioni 4.5 katika sekta ya elimu, afya, maji, uwekezaji na minundombinu ya barabara.
Hata hivyo Mkurugenzi Msumi, ameahidi kuendelea kufanyia kazi maagizo na ushauri uliotolewa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa ndugu Sahili Nyanzabara Geraruma, ili kufikia malengo yaliyowekwa na serikali kwa maendeleo ya wananchi Arusha na taifa kwa ujumla.
Kauli Mbiu: ya Mwenge wa Uhuru 2022, ni SENSA NI MSIMGI WA MIPANGO YA MAENDELEO: SHIRIKI KUHESABIWA, TUYAFIKIE MAENDELEO.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.