Na. Elinipa Lupembe
Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi, amekabidhi sadaka ya Eid kwa watoto yatima wa kituo cha Rahma Orphanage, kilichopo eneo la Ngaramtoni kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu.
Mkurugenzi Msumi amekabidhi sadaka hiyo pamoja na kutoa salamu maalum za Eid Al Hajj kwa niaba ya Mheshimiwa Rais, ambaye amewatakia watoto hao Kheri ya sikukuu ya Eid Al Hajj, na kuwataka kuishi kwa amani na upendo huku wakitambua ya kwamba, bibi yao mama Samia anawapenda, anawajali na kuwathamini sana kama watoto wengine.
Ameongeza kuwa Mheshimiwa Rais anawathamini sana watoto yatima, na anapenda waishi maisha mazuri kama watoto wengine wa kitanzania huku akiitaka jamii kushiriki kuwahudumia watoto hao, ili waweze kutimiza ndoto zao.
"Mheshimiwa Rais anawajali watanzania wote na amewiwa kutoa sadaka hii kwa ajili yenu, anataka mjisikie wenye furaha katika kusherehekea sikukuu ya Eid Al Hajj kama watoto wengine" amesisitiza Msumi.
Hata hivyo watoto hao, wamefurahishwa sana na kitendo hicho cha kiungwana kilichofanywa na mheshimiwa Rais, licha ya kumshukuru wamemuombea dua njema ya kumtakia kheri ya Sikukuu, kumuombea kheri katika maisha yake na hata katika kutekeleza majukumu yake ya kuiongoza nchi yao ya Tanzania.
Akizungumza kwa niaba ya watoto hao, Zakia Ibrahimu, amemshukuru mama Samia na kumtaka aendelee na moyo huo wa upendo wa kuwajali watoto hususani watoto yatima, watoto ambao wanafarijika sana, wanapoona jamii inawajali na kuwathamini.
Naye Katibu wa jumuia ya wanawake DHI NUREYN Islamic Foundation, Hodhan Ally, licha ya kumshukuru mama Samia ameipongeza serikali ya awamu ya sita kwa kuwajali watoto yatima na hakusita kumuombea dua jema Mheshimiwa Rais, huku akimtakia kila lenye kheri katika kuiongoza nchi.
"Watoto hawa wanafarijika sana pale wanapoona serikali na hasa kiongozi mkubwa kama Rais anawakumbuka yatima, watoto wanapata amani mnoo wageni wakija kuwaona, hata dini inahimiza kuwajali na kuwapenda yatima, hii ni ibada yenye thawabu kubwa kwa Mwenyenzi Mungu ambayo Mama Samia ameifanya kwa watoto hawa, tunamshukuru sana, Alhamdulilah " Amesisitiza Mama Hodhan.
Naye Afisa Ustawi wa Jamii, halmashauri ya Arusha, Beatrice Tengi, ametaja sadaka iliyotolewa na mheshimiwa rais ni pamoja na mbuzi, Kilo 50 za unga, mchele na sukari, juisi, pipi, sabuni, Lita 20 za mafuta ya kula, mafuta ya kujipaka, miswaki na dawa za meno, vyenye thamani ya shilingi laki 8.
Kituo cha Rahma Ophanate, kinasimamiwa na Jumuia ya Islamic Foundation, na kinalea jumla ya watoto yatima 26, kikiwa miongoni mwa vituo viwili vya kulea watoto Yatima mkoa wa Arusha, vilivyopewa sadaka ya Eid na Mheshimwa Raisi Samia Suluhu Hassan .
Waislamu nchini wameungana na waislamu wote duniani kushehekea sikukuuu ya Eid Al Hajj, ambayo husherehekewa baada ya kutamatika kwa ibada ya Hijja, ibada inayohitaji mtu kuwa mzima wa kimwili na uwezo wa kifedha wa kuweza kufanya ibada hiyo angalau mara moja katika maisha ya muumini.
EID AL ADHA MUBARAKA
ARUSHA DC - KaziInaendelea
JIANDAE KUHESABIWA
PICHA ZA MATUKIO WAKATI MKURUGEZNI AKIKABIDHI SADAKA KWA WATOTO YATIMA
Mkurugenzi Mtenzaji halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi akikabidhi kilo 50 za Sukari kwa watoto yatima wa kituo cha Rahma Orphanage cha Ngaramtoni, Sadaka iliyotolewa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kupitia Ofisi ya waziri Mkuu.
Mkurugenzi Mtenzaji halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi akikabidhi katoni ya mafuta ya kujipaka kwa watoto yatima wa kituo cha Rahma Orphanage cha Ngaramtoni, Sadaka iliyotolewa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kupitia Ofisi ya waziri Mkuu.
Mkurugenzi Mtenzaji halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi akikabidhi lita 20 za mafuta ya kupikia kwa watoto yatima wa kituo cha Rahma Orphanage cha Ngaramtoni, Sadaka iliyotolewa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kupitia Ofisi ya waziri Mkuu.
Mkurugenzi Mtenzaji halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi akikabidhi boksi la biskuti kwa watoto yatima wa kituo cha Rahma Orphanage cha Ngaramtoni, Sadaka iliyotolewa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kupitia Ofisi ya waziri Mkuu.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.