Na Elinipa Lupembe.
Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi, amekanidhiwa gari lenye namba za usajili STM 5616, kutoka kwa Afisa Elimu Sekondari mara baada ya kukabidhiwa gari hilo na Waziri wa Nchi OR - TAMISEMI jijini Dar - es - Salaam mwishoni wa wiki iliyopita.
Mkurugenzi Msumi, amethibitisha kupokea gari la idara ya elimu sekondari, kwa kuipongeza na kuishukuru serikali kwa kuona umuhimu wa kutoa kitendae kazi hicho muhimu kwa Idara ya Elimu.
"Gari hili litawezesha kuwafikia walengwa ambao ni walimu na wanafunzi katika ufauatilia wa shughuli za kitaaluma pamojan na utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika ya idara hiyo ya elimu". Amefafanua
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Arusha, Mhe. Ojung' Salekwa, kwa niaba ya wananchi wa halmashauri hiyo, ametumia fursa hiyo kuishukuru serikali ya awamu ya sita, inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kuleta vitendea kazi katika halmashauri hiyo na kuahidi kusimamia utunzaji na matumizi yake, ili kufikia lengo lililokusudiwa na serikali.
Hata hivyo, Mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari halmashauri ya Arusha, Mwl. Menard Lupenza, amesema kuwa uwepo wa gari kwenye idara, utarahisisha shughuli za ufuatiliaji wa taaluma na miradi ya maendelo shule.
"Licha ya kufika malengo ya serikali, gari hili litatuwezesha kufikia malengo ya halmashauri tuliyojiwekea, kuwa zaidi ya asilimia 50 ya wanafunzi kupata daraja la kwanza mpaka la tatu, ikiwa ni kampeni ya kutokomeza 'zero'". Amebainisha Mwl. Lupenza
Awali Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, imenunua magari 200 ambapo magari 95 yameshagawiwa kwa halmashauri nchini kwa awamu tatu, halmashauri ya Arusha ikiwa ni miongoni.
Ikumbukwe kuwa, uwepo wa vitendea kazi katika sekta ya elimu ni sehemu ya uboreshaji wa miundo mbinu na huduma za elimu, ikiwa ni uweshaji mazingira rafiki ya kujifunzia na kufundishia kwa walimu na wanafunzi ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ( CCM) ya mwaka 2022- 2025.
"ARUSHA DC ni yetu, Tushirikiane Kuijenga"
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.