• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

DED ARUSHA DC AWATAKA MAAFISA WATENDAJI WA KATA KUANDAA MPANGO WA MAENDELEO WA KATA UNAOTEKELEZEKA

Posted on: July 29th, 2020

  Na. Elinipa Lupembe.
       Maofisa Watendaji wa Kata, halmashauri ya Arusha wametakiwa kuandaa Mpango wa Maendeleo wa kata, unaotekelezeka na unaoendana na mahitaji ya wananchi ili kuweka malengo makakati ya utekelezaji wa mapngo huo, kwa maendeleo wananchi wa kata hizo.
      Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha, Saad Mtambule, alipofanya ziara yake ya kwanza ya kikazi ya kutembelea Ofisi za kata za halmashauri hiyo, kujionea  utendaji kazi wa ofisi hizo, pamoja na uibuaji wa miradi ya maendeleo katika maeneo hayo.
      Mkurugenzi huyo, amewataka Maofisa Watendaji zote za halmashauri hiyo, kuwa na Mpango wa Maendeleo kisekta, unaotokana na maoni na mapendekezo ya wananchi, ukijikita kwenye changamoto zinazoikabili jamii husika pamoja na mipango mkakati wa kuzitatua kwa kuzingati vipaumbele vya wananchi hao.
     Aidha amefafanua kuwa, Mpango huo wa Maendeleo, utawezesha kuandaa bajeti ya mwaka kulingana na mahitaji ya jamii,hasa kwa kuzingatia vipaumbele vya wananchi wa maeneo hayo.
     "Mpango wa Maendeleo wa Kata ndio Dira ya Maendeleo ya Kata, utakaowezesha Maofisa Watendaji wote, kupanga utekelezaji wa shughuli zote za maendeleo kwa mwaka na kufanya tathmini  yakufahamu mwelekeo wa maendeleo walipotoka, walipo na malengo wanayotarajia kufikia kwa kuzingatia maendeleo ya kiuchumi na kijamii" amesisitiza Mkurugenzi huyo.
     Ameendelea kufafanua kuwa Mpango huo wa Maendeleo, utawawezesha wananchi pia kufahamu vema dira ya maendeleo katika maeneo yao, na kujipanga namna ya kushiriki kutatua changamoto zinazowakabili kwa kuzingatia vipaumbele vyao na Taifa kwa ujumla.
      Aidha amewataka Watendaji hao kukaa na Watendaji wa vijiji pamoja na  wataalam wote wa ngazi hizo, kuandaa Mpango huo wa Maendeleo kisekta, kwa kuzingatia mahitaji ya wananchi katika maeneo yao, sambamba na kupata maoni kupitia wajumbe wa serikali za vijiji na mikutano ya vijiji.
     Naye Kaimu Afisa Mipango, halmashauri ya Arusha, Albert Mahoo, Mpango wa Maendeleo ya kata unaanza kwa kukusanya mapendekezo ya mahitaji ya  wananchi kisekta kupitia mikutano ya vitongoji na vijiji, kisha kuandaa mpango huo kupitia ofisi za kata kwa kuzingatia mpango halisi wa bajeti na vipaumbele kisekta.
    Hata hivyo Mahoo, amewataka wananchi wa halmashauri hiyo, kujijengea tabia ya kuhudhueia na kushiriki kwenye mikutano ya vijiji na vitongoji katika maeneo wanayoishi, ili kuweza kujipangia mipango ya maendeleo katika maeneo yao na kuweza kufuatilia kwa karibu, utekelezaji wa mipango hiyo wakati wa mikutano hiyo.
  "Mikutano ya Vitongoji na Vijiji ni kwa ajili ya wananchi wote wakazi wa maeneo husika kwa ajili ya kupanga mipango ya maendeleo katika maeneo yao na kufuatilia utekelezaji wake, bila kujali nafasi zao, hali za kimaisha wala itikadi za kidini za za kisiasa" amesisitiza Kaimu Afisa Mpiango huyo.

      Ameomgeza kuwa, Mpango huo wa maendeleo, utawawezesha Watendaji wa kata na vijiji kuandaa bajeti inayoendana na mahitaji ya jamii husika na kurahisisha ushiriki wa jamii katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo katika maeneo yao, na kufungua njia kwa wadau wa maendeleo kushiriki utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika maeneo husika.
      Awali Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha, amefanya ziara ya kutembelea kata za Moivo, Oloirieni na Olturumet lengo likiwa kuhakikisha utendaji wa kazi kuanzia ngazi ya kata, uendane na Mipango wa maendeleo wa halmashauri na taifa.







Matangazo

  • TANGAZO LA KAZI ZA MKATABA HALMASHAURI YA WILAYA YA ARUSHA August 14, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • KUFUATILIA NA USAMIZI WA HAKI ZA MTOTO KATIKA JAMII NI JAMBO MUHIMU

    August 25, 2025
  • RAIS SAMIA AMUAPISHA AMOS MAKALLA KUWA MKUU WA MKOA WA ARUSHA

    August 26, 2025
  • DKT. JAHANNES LEMBULUNG' LUKUMAY ACHUKUWA FOMU YA UGOMBEA UBUNGE WA CCM JIMBO LA ARUMERU MAGHARIBI

    August 25, 2025
  • KIKAO KAZI CHA WENYEVYITI WA BODI NA WATENDAJI WAKUU WA TAASISI ZA UMMA (CEOs Forum 2025)

    August 24, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.