• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

DED Arusha DC awataka watumishi kufanya kazi kwa weledi

Posted on: February 8th, 2019

Na. Elinipa Lupembe

Watumishi halmashauri ya Arusha, wametakiwa kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kwa ushirikiano bila kubaguana kwa vyeo wala nafasi walizonazo, ili kufikia malengo ya halmashauri yaliyoaanishwa kwenye mpango mkakati wa halmashauri hiyo, malengi yaliyojikita zaidi katika kuwatumikia wananchi.

Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Arusha Dkt. Wilson Mahera, katika kikao kazi cha kawaida, kinachowakutanisha watumishi wote wa makao makuu ya halmshauri hiyo, kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya Arusha.

Mkurugenzi Mahera, amesema kuwa kikao hicho kina lengo la kukumbusha watumishi haki na wajibu wao katika kufanya kazi za utumishi wa umma, kazi zilizojikita zaidi katika kuzingatia kanuni, sheria, taratibu na miongozo ya serikali.

Amesema kuwa kila mtumishi ana haki sawa na anatakiwa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma, katika kutekeleza majukumu yake ya kila siku, kufanya kazi kwa weledi na kutumia taaluma yake aliayosomea kwa kushirikiana na watumishi wenzake ili kufikia malengo ya serikali.

Aidha amewataka watumishi hao kukaa pamoja na kujadili changamoto zinazowakabili katika kutekeleza majukumu yao, ikiwa ni pamoja na kuweka wazi kero walizo nazo ili ziweze kutatuliwa kwa wakati na menejimenti, badala ya kusubiri mpaka mambo yaharibike ndipo kuaza kulalamika.

Hata hivyo Dkt. Mahera amesisitiza kuboreshwa kwa dawati la malalamiko na kero katika halmshauri hiyo na kusisitiza kuwa malalamiko yote kushughulikiwa na idara husika kwa usimamizi wake, huku akiwataka watumishi noa pia kutumia dawati hilo kufikisha malalamiko yao ili yaweze kutatuliwa kwa wakati na kutambua kuwa dawati hilo si la wananchi peke yao.

“Dawati la malalamiko si la wananchi peke yao, hata ninyi watumishi linawahusu, unapopata tatizo lililoshindikana ndani ya idara au kitengo chako, wasilisha  kwenye dawati hilo, ndio sehemu sahihi na litashughulikiwa kwa wakati, badala ya kulalamika huko jambo ambalo linaeneza chuki baina yetu” amesema Mkurugenzi huyo.

Naye Mkuu wa Idara ya Utumishi, halmashauri ya Arusha Hamis Mpume, amewaahidi watumishi hao kuendelea kusimamia haki zao, wajibu na usawa, na kuwakumbusha watumishi hao kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa kuzingatia maadili ya utumishi wa Umma ikiwa ni apamoja na kutekeleza wajibu wao na kuahidi kuwachukulia hatua watakaokwenda kinyume.

“Nina imani kila mtumishi anafahamu vizuri majukumu yake, niwatake kila mmoja wenu kuyatekeleza kwa ufanisi, mimi kama msimamizi wenu, nitatenda haki, sitamuonea mtu ila sitasita kumchukulia hatua stahiki yule  asiotekeleza majukumu yake"  amesema Mpume

Ameongeza kuwa, kuna haja ya kukutana na watumishi kila Ijumaa ya mwisho wa mwezi pamoja na kufanyika vikao vya idara na vitengo kila mwezi ili kushughulikia matatizo ya watumishi kwa wakati.

Hata hivyo watumishi hao, wameahaidi kutekeleza majukumu yao kama walivyosaini kwenye mikataba yao ya utumishi wa Umma na kumuomba mkurugenzi wao, kuwapa motisha katika utekel;ezaji wa majukumu yao, motisha ambayo huwaongezea ari ya kufanya kazi.

Simon Mwanjwangwa ambaye na Mhasibu wa halmashauri hiyo, licha ya kumshukuru Mkurugenzi huyo kwa kukaa pamoja na kujadili changamoto zinazowakabili amemuomba mkurugenzi huyo kutoa motisha chanya kwa watumishi pale wanapofanya kazi, jambo ambalo linawaongezea ari ya kufanya kazi pamoja na kupenda kazi yao.










Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.