• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

DED ARUSHA DC: MWAKA 2023 TUSHIRIKIANE KUIFANYA ARUSHA DC YA KIJANI KWA KUPANDA MITI

Posted on: April 15th, 2023

Na Elinipa Lupembe

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha,  Seleman Msumi, amewataka wanachi wa halmashauri hiyo kushirikiana kuifanya Arusha DC, kuwa ya kijani kama ilivyokuwa miaka ya nyuma kwa kila mkazi kupanda miti.

Mkurugenzi huyo ametoa rai hiyo, wakati wa zoezi la upandaji miti shule ya msingi Bwawani kata ya Bwawani, ikiwa  ni siku ya nne ya Kampeni ya upandaji miti, mwaka 2023 katika halmashauri hiyo.

Amefafanua kuwa kama halmashauri tukiweka nia ya dhati, tunao uwezo mkubwa wa kuifanya Halmashauri yetu kuwa ya kijani, kwa kupanda miti kwa wingi kwa kuhusisha kila mtu kuanzia mtoto mpaka mzee.

"Kila mtu kwenye familia akipanda miti mitano kila mwaka na kuitunza vizuri, Arusha itakuwa ya kijani na itarejesha uoto wake wa asili, tuliouharibu, hilo liko ndani ya uwezo wetu, sisi kama Serikali kwa kushirikiana na wadau, tunatoa miti kwenye vijiji vilivyoathirika zaidi, tumieni fursa hiyo" Amebainisha Msumi.

Ameyataja matokeo ya ukame ambayo wanaArusha tumeanza  kuyashuhudia ikiwemo upungufu wa mvua, zaidi mvua kunyesha tofauti na msimu, jambo linalosababisha ukame kwenye halmashauri na maeneo mengi katika nchi yetu.

Aidha amewasisitiza wananchi kuona umuhimu wa kampeni hii ya upandaji miti na kufafanua kuwa, kupanda miti ni jambo muhimu lakini kuitunza miti nia jambo muhimu na kubwa zaidi, hivyo kila mtu aliyepanda mti kuhakikisha anautunza ili ukue.

Diwani wa kata ya Bwawani Mhe. Mollel, licha ya kuushukuru uongozi wa halmashauri kwa kuendesha zoezi la upandaji miti katani kwake, ameahidi kushirikiana na viongozi wa vijiji na vitongoji kuhakikisha wananchi wanapanda miti na kuitunza.

Mhe. Diwani huyo amekiri uwepo wa uharibifu wa mazingira uliosababishwa na ukataji miti, lakini amekiri kuwa serikali za vijiji za kata yake, kwa miaka miwili sasa wameanza utatatibu wa usimamizi wa sheria ndogo za utunzaji wa mazingira, licha ya changamoto ya mifugo

"Nikutoe hofu, mkurugenzi na wadau wetu, miti hii tutaendelea kuisimamia na kuhakikisha wananchi wameiotesha kwenye maeneo yao, na kusimamia ukuaji wake, kwa kuwa tunayo sheri ya mtu anayeharibu mti uliopandwa na hata mifugo yake kula miti" . Mhe Diwani


"Mti wangu, Taifa langu, Mazingira yangu, KaziIendelee"

Matangazo

  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MKUTANO WA BARAZA LA MADIWANI WA ROBO YA TATU 2O21/2022 tarehe 09.05.2022 May 08, 2022
  • Tazama zote

Habari mpya

  • MKURUGENZI WA ARUSHA DC,BW.SELEMAN MSUMI AKIWA NA WATUMISHI WA HALMASHAURI HIYO KATIKA MASDHIMISHO YA MEI MOSI KIMKOA ARUSHA

    May 02, 2025
  • HERI YA MEI MOSI

    May 01, 2025
  • HERI YA SIKU YA MEI MOSI

    May 01, 2025
  • MHE. MAJALIWA MGENI RASMI KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI DUNIANI

    April 29, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.