Na Elinipa Lupemne
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi, amezindua ujenzi wa miundombinu ya elimu kwa shule za msingi, mradi unaotekelezwa na serikali kupitia mradi ya BOOST.
Mkurugenzi Msumi, amezindua utekelezaji wa miradi hiyo kwa kujumuika na wananchi wa Kijiji cha Lemanda kuchimba msingi wa majengo ya shule mpya ya msingi kijiji cha Lemanda, shule ambayo wameipa jina la Naisula.
Akizungumza wakati wa kuzindua ujenzi wa majengo hayo, Mkurugenzi Msumi licha ya kuishukuru serikali, ameweka wazi kuwa miradi hiyo ni muhimu kwa wanafunzi wa halmashauri hiyo, kutokana na changamoto kubwa ya uchakavu wa majengo kwenye shule za msingi.
"Tumepokea shilingi milioni 682.5, fedha zitakazohusisha ujenzi wa miundombinu kwa shule 6 za msingi, Miradi hii italeta mapinduzi makubwa kwa watoto wa wafugaji, wanaoshi maeneo ya pembezoni, miradi itakayokwenda kutekeleza malengo ya serikali ya kuondoa tatizo la Kusoma, Kuandika na Kuhesabu.
Hata hivyo mkurugenzi Msumi, amewataka wananchi wa maeneo yote inayotekelezwa miradi hiyo kwa kushirikiana na watalamu katika utekelezaji wa miradi hiyo kutambua kuwa miradi hiyo ni mali yao.
Ikumbukwe kuwa, miradi hiyo ya ujenzi wa miundombinu shule za msingi ni utekelzaji wa Ilani ya CCM, Sura ya tatu Ibara ya 79 kifungu (q)Kukarabati miundombinu ya kufundishia na kujifunzia na kifungu (C)Kuboresha uratibu na usimamiaji wa stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu.
ARUSHA DC ni Yetu, Tushirikiane Kuijenga"
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.