• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

DED ARUSHA DC AZINDUA UJENZI WA KITUO KIPYA CHA AFYA OLOIRIENI

Posted on: October 6th, 2021

Na. Elinipa Lupembe

Mkurugenzi mtendaji halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi, amezindua rasmi ujenzi wa kituo kipya  cha Afya cha Oloirieni, kinachojengwa katika kata ya Oloirieni, mradi unaotekelelezwa na halmashauri kupitia fedha za fidia ya deni la  Lakilaki, mradi utakaogharimu kiasi cha shilingi milioni 450.

Katika uzinduzi huo, mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, amefanya ishara ya kuanzisha uchimbaji wa msingi wa majengo matatu  ya kituo kituo hicho kipya cha afya, tukio lililoshuhudiwa na wakazi wa kitongoji cha Oloirieni, wajumbe wa kamati ya ujenzi wa kituo hicho cha afya, watalamu wa ngazi ya kata na ngazi ya halmashauri ikijumuiasha Wakuu wa Idara na Vitengo, zoezi lililofanyika kwenye kitongoji cha Oloirien ambapo mradi huo umeanza kutekelezwa.

Mkurugenzi Msumi, amewataka wananchi wa Oloirieni kutambua kuwa mradi huo ni mali yao, hivyo wanajukumu kubwa la kushiriki katika usimamizi wa mradi huo katika hatua zote za ujenzi kama taratibu za forced akaunti unavyoelekeza, pamoja na kuhakikisha ulinzi wa vifaa vyote vinavyoletwa katika eneo hilo la ujenzi huku akwataka wajumbe wa kamati ya ujenzi kuhakikisha wanasimamia vema hatua zote za utekelezaji wa mradi huo.

"Kamati ya ujenzi, mmepewa dhamana na wananchi wenzenu ya kusimamia ujenzi wa kituo chao cha afya, hakikisheni mnasimamia kwa kufuata taratibu zote za ujenzi, kama zinavyoelekezwa na serikali, ili muweze kupata majengo yenye ubora kulingana na thamani ya pesa, tambueni fedha hizo ni kodi za wananchi, kuweni wazalendo katika usimamizi wa mradi huu utakaotumia fedha nyingi za umma" amesisitiza Mkurugenzi Msumi.

Ameongeza kuwa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimwa Rais, mama Samia Suluhu Hassan, inawajali wananchi wake, kwa kutekeleza mkakati wake wa kuhakikisha kila kata inakuwa na kituo cha afya chenye hadhi ya nyota tano, lengo kubwa likiwa ni kusogeza huduma za afya karibu na wananchi pamoja na kutokomeza vifo vya kina mama na watoto wakati wa kujifungua.

Naye Afisa Mipango, halmashauri ya Arusha, Anna Urio amebainisha kuwa kiasi hicho cha shilingi milioni 450 kitatumika kujenga majengo matatu ikiwemo jengo la wagonjwa wa nje 'OPD', jengo la mama na mtoto 'martenity word', jengo la maabara, kichomea taka 'incinerator' na kusisitiza  kuwa mradi huo unategemea kukamilika mwishoni mwa mwaka huu wa 2021.

Hata hivyo wananchi wa kata ya Oloirieni wameishukuru serikali kwa kuwakumbuka na kuwajengea kituo cha afya, jambo ambalo lilikuwa ni ndoto katika kata hiyo, na kuthibitisha kuwa, uwepo wa kituo hicho cha afya, utawewezesha kupata huduma bora za afya ndani ya eneo la kata yao, jambo ambalo litawapunguzia gharama za usafiri na gharama za matibabu, tofauti na hapo awali walikwenda kutibiwa katika hospitali ya wilaya ya olturumeti ama Seliani Ngaramtoni ambayo ni  hospitali ya kulipa.

Mwenyekiti wa kitongoji cha Oloirieni mheshimiwa John Aminiel, amepongeza juhudi za serikali ya kuweka kipaumbele katika uboreshaji wa miundo mbinu ya afya nchini, huku utekelezaji wa Ilani ya CCM ya kuhakikisha kila kata inakuwa na kituo cha afya chenye hadhi ya nyota tano.

Mwenyekiti wa kamati ya ujenzi, Ismail Marunda licha ya kuishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuwapatia mradi wa kituo cha afya katika kata yao, mradi ambao ameutaja kuwa ni wa muhimu sana kwa wakazi wa kata ya Oloirieni na majrani zao, na kuahidi kusimamia vema hatua zote za utekelezaji wa ujenzi wa kituo hiko ili kufikia malengo ya serikali ya kuwa na kituo bora cha afya.

Naye Sesilia Vanica, mwenyekiti wa kamati ya mapokezi  ameweka wazi kuwa uwepo wa kituo cha afya katika kata ya Oloirieni utawanufaisha sana wanawake wa eneo hilo, kwa kuwa wananwake ndio waathirika wakubwa wa huduma za afya kwa familia zao na kuongeza kuwa kituo hicho kitapunguza vifo visivyo vya lazima hasa kwa wanawake wajawazito na watoto wa chini ya miaka mitano.

"Kwa sasa inatulazimu kwenda kutibiwa hospitali ya serikalia ya Olturumeti, hospitali ambayo iko mbali sana kutoka hapa, licha ya kuwa hapa jirani kuna hospitali ya binafsi kitu ambacho wananchi wengi hushindwa kwenda kwenye hospitali hiyo kwa kuwa hawana uwezo wa kifedha kugharamia matibabu, lakini uwepo wa kituo hicha cha serikali, kitaokoa maisha ya watu wengi hata wasio na uwezo kifedha" Amesisitiza Selilia.

Baaada ya kukamilika kwa ujenzi wa kituo hicho cha Afya, inakadiriwa kuhudumia takribani wagonjwa elfu 14 wa kata ya Oloirieni na vitongoji vyake pamoja na vitongoji vingine vya kata jirani.



MATUKIO KATIKA PICHA


Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha Seleman Msumi, akichimba msingi kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa Kituo kipya cha afya cha Oloirieni, mradi unaotekelezwa na fedha za Lakilaki kwa gharama ya shilingi milioni 450.


Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha Seleman Msumi, akizungumza na wananchi wa kitongoji cha Oloirien, wakati wa uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa Kituo kipya cha afya cha Oloirieni, mradi unaotekelezwa na fedha za Lakilaki kwa gharama ya shilingi milioni 450.


Afisa Mipango, halmashauri ya Arusha Anna Urio, akichimba msingi kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa Kituo kipya cha afya cha Oloirieni, mradi unaotekelezwa na fedha za Lakilaki kwa gharama ya shilingi milioni 450.

Mwenyekiti wa kitongoji cha Oloirieni mheshimiwa John Aminiel, akichimba msingi kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa Kituo kipya cha afya cha Oloirieni, mradi unaotekelezwa na fedha za Lakilaki kwa gharama ya shilingi milioni 450.


Afisa Elimu Msingi, halmashauri ya Arusha, mwalimu Hossein Mghewa, akichimba msingi kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa Kituo kipya cha afya cha Oloirieni, mradi unaotekelezwa na fedha za Lakilaki kwa gharama ya shilingi milioni 450.

Wananchi wa kata ya Oloirini waliojitokeza kwenye uzinduzi, mradi wa ujenzi wa Kituo kipya cha afya cha Oloirieni, mradi unaotekelezwa na fedha za Lakilaki kwa gharama ya shilingi milioni 450.


MICHORO YA MAJENGO YA KITUO KIPYA CHA AFYA CHA OLOIRIENI


Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.