Na. Elinipa Lupembe.
Mkurugenzi mtendaji halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi, amezindua rasmi ujenzi wa kituo kipya cha Afya cha Oloirieni, kinachojengwa katika kata ya Oloirieni, mradi unaotekelelezwa na halmashauri kupitia fedha za fidia ya deni la Lakilaki, mradi uatakaogharimu kiasi cha shilingi milioni 450.
Katika uzinduzi huo, mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, amefanya ishara ya kuanzisha uchimbaji wa msingi wa majengo matatu ya kituo kituo hicho cha afya, tukio lililoshuhudiwa na wakazi wa kitongoji cha Oloirieni, wajumbe wa kamati ya ujenzi wa kituo hicho cha afya, watalamu wa ngazi ya kata pamoja na wakuu wa Idara na Vitengo, zoezi lililofanyika kwenye kitongoji cha Oloirien ambapo mradi huo unatekelezwa.
Mkurugenzi Msumi, amewataka wananchi wa Oloirieni kutambua kuwa mradi huo ni mali yao, hivyo wanajukumu kubwa la kushiriki katika hatua zote za utekelezaji wa mradi huo, ikiwemo usimamizi wa mradi huo katika hatua zote kama taratibu za forced akaunti unavyoelekeza, pamoja na kuhakikisha ulinzi wa vifaa vyote vinavyoletwa katika eneo hilo la ujenzi huku akwataka wajumbe wa kamati ya ujenzi kuhakikisha wanasimamia vema hatua zote za utekelezaji wa mradi huo.
"Kamati ya ujenzi, mmepewa dhamana na wananchi wenzenu ya kusimamia ujenzi wa kituo chao cha afya, hakikisheni mnasimamia kwa kufuata taratibu zote za ujenzi, kama zinavyoelekezwa na serikali, ili muweze kupata majengo yenye ubora kulingana na thamani ya pesa, tambueni fedha hizo ni kodi za wananchi, kuweni wazalendo katika usimamizi wa mradi huu wenye fedha nyingi za umma" amesisitiza Mkurugenzi Msumi.
Ameongeza kuwa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimwa Rais, mama Samia Suluhu Hassan, inawajali wananchi kwa kutekeleza mkakati wake wa kuhakikisha kila kata inakuwa na kituo cha afya chenye hadhi ya nyota tano, lengo kubwa ikiwa ni kusogeza huduma za afya karibu na wananchi pamoja na kutokomeza vifo vya kina mama na watoto wakati wa kujifungua.
Naye Afisa Mipango, halmashauri ya Arusha, Anna Urio amebainisha kuwa kiasi hicho cha shilingi milioni 450 kitatumika kujenga majengo matatu ikiwemo jengo la wagonjwa wa nje 'OPD', jengo la mama na mtoto 'martenity word', jengo la maabara, kichomea taka 'incinerator' na kuongeza kuwa maradi huo unategemea kukamilika mwisho mwa mwaka huu wa 2021.
Hata hivyo wananchi wa kata ya Oloirieni wameishukuru serikali kwa kuwakumbuka na kuwajengea kituo cha afya, jambo ambalo lilikuwa ni ndoto katika kata hiyo, na kuthibitisha kuwa, uwepo wa kituo hicho cha afya, utawewezesha kupata huduma bora za afya ndani ya eneo la kata yao, jambo amabalo litawapunguzia gharama za usafiri, tofauti na hapo awali walikwenda kutibiwa katika hospitali ya wilaya ya olturumeti ama Seliani Ngaramtoni.
Mwenyekiti wa kamati ya ujenzi, Ismail Marunda licha ya kuishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuwapatia mradi wa kituo cha afya katika kata yao, mradi ambao ameutaja kuwa ni wa muhimu sana kwa wakazi wa kata ya Oloirieni na majrani zao .
Naye mwenyekiti wa kamati ya mapokezi Sesilia Vanica, ameweka wazi kuwa uwepo wa kituo cha afya katika kata ya Oloirieni utawanufaisha sana wanawake wa eneo hilo, kwa kuwa wananwake ndio waathirika wakubwa wa afya za familia zao na kuongeza kuwa kituo hicho kitapunguza vifo visivyo vya lazima hasa kwa wanawake wajawazito na watoto wa chini ya miaka mitano.
"Kwa sasa inatulazimu kwenda kutibiwa hospitali ya serikali ya Olturumeti, hospitali ambayo iko mbali sana kutoka hapa, licha ya kuwa hapa jirani kuna hospitali ya binafsi kitu ambacho wananchi wengi hushindwa kwenda kwenye hospitali hiyo kwa kuwa hawana uwezo wa kifedha kugharamia matibabu, lakini uwepo wa kituo hicha cha serikali, kitaokoa maisha ya watu wengi hata wasio na uwezo kifedha" Amesisitiza Selilia.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi, akichimba msingi, kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa kituo kipya cha Afya Oloirieni kata ya Oloirieni.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi, akizungumza na wananchi wa kata ya Oloirieni mara baada ya uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa kituo kipya cha Afya Oloirieni kata ya Oloirieni.
Mwenyekiti wa kitongoji cha Oloirieni, Mheshimiwa ...... akichimba msingi, kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa kituo kipya cha Afya Oloirieni kata ya Oloirieni.
Afisa Mipango Halmashauri ya Arusha, Anna Urio, akichimba msingi, kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa kituo kipya cha Afya Oloirieni kata ya Oloirieni.
Afisa Elimu Msingi Halmashauri ya Arusha, mwalimu Hossein Mghewa, akichimba msingi, kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa kituo kipya cha Afya Oloirieni kata ya Oloirieni.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa kituo cha Afya Oloirieni Ismail Marunda, akichimba msingi ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa maradi wa ujenzi wa Kituo Kipya cha Afya cha Oloirieni.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.