TANGAZO TANGAZO: 13/01/2023
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Babati Wilaya, anapenda kuwatangazia wananchi kuwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu vilivyo na sifa ya kupata Mkopo isiyo na riba kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023, kwa robo ya tatu (Januari-March),Halmashauri inapokea maombi ya mikopo isiyo na riba.
Maombi yanafanyanyika kupitia mfumo wa Ki-electronic wa TPLMIS (https:mikopohalmashauri.tamisemi.go.tz/login) kwa,kutumia simu Janja na ‘Computer’ zinatumika katika maeneo yetu ya Kata na Vijiji. Maafisa Maendeleo ya Jamii wapo katika Tarafa zote kwa ajili ya uwezeshaji wa usajili na maombi ya mikopo kwa kutumia mfumo. Halmashauri imetenga kiasi cha Tsh: 236,940,000/= kwa mwaka wa fedha 2022/2023, ikiwa ni 10% ya mapato ya ndani. Viambatisho vyote vya maombi vilivyopitia Kamati ya Maendeleo ya Kata, vitumike kama mnavyoelekezwa na Maafisa Maendeleo ya Jamii.
MAHITAJI YA USAJILI WA VIKUNDI KATIKA MFUMO.
Kusajili katika Mfumo wa ‘Ten Percent Loan management information
System’ (TPL-MIS) (https:mikopohalmashauri.tamisemi.go.tz/login).
1. Kikundi Kiwe na email address.
2. Kila mwanakikundi awe na Namba za NIDA au Kitambulisho cha NIDA
na namba ya simu ya kila mwanakikundi.
3. Kikundi kiwe na Katiba.
4. Kikundi kiwe na mradi wa pamoja/ wazo la mradi.
5. Kikundi lazima kiwe na akaunti namba.
6. Idadi ya wanachama wa vikundi vya Wanawake na Vijana ni kuanzia
watu watano (5) na kuendelea Walemavu kuanzia watu (2) hadi watu
watano (5).
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.