DKT. BITEKO AWASILI NCHINI INDIA KWA ZIARA YA KIKAZI
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko Februari 11, 2025 amewasili nchini India kwa ajili ya kushiriki mikutano mbalimbali ya kimataifa ya nishati ambayo inaenda sambamba na Maadhimisho ya Tatu ya Wiki ya Nishati ya India mwaka 2025 (India 3rd Annual Energy Week) kuanzia tarehe 11 hadi 14 Februari, 2025.
Katika Uwanja wa Kimataifa wa Indira Gandhi, jijini New Delhi, Dkt.Biteko amepokelewa na Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Anisa Mbega na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Mafuta na Gesi India, Sandeep Jain.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.