OR TAMISEMI
Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Dkt. Festo Dugange ameipongeza halmashauri ya wilaya Arusha kwa ubuniufu wa kujenga majengo ya shule kwa kutumia michoro ya ghorofa katika shule ya sekondari mpya ya Kiutu.
Ametoa pongezi hizo tarehe 08 Machi 2023 wakati akikagua ujenzi wa Shule Mpya ya Kiutu inayojengwa kupitia Mradi wa kuboresha Elimu ya Sekondari (SEQUIP).
Dkt. Dugange amesema kutokana na ufinyu wa eneo inapojengwa shule, halmashauri iliamua kujenga baadhi ya majengo kwa mfumo wa ghorofa ambapo ameridhishwa na hali ya ujenzi inayoendelea.
Amesema Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alitoa shilingi milioni 470 za awali na halmashauri kupitia mapato ya ndani ilitoa milioni 250 ili kuwezesha ujenzi wa shule hiyo unaoendelea.
Aidha, Dkt. Dugange ameeleza kuwa kutokana na makadilio ya awali zinahitajika shilingi milioni 111 ili kukamilisha ujenzi wa mradi huo ambapo makadilio ya gharama za ujenzi wa Mradi huo zilikuwa shilingi milioni 696.
Kutokana na gharama za ujenzi na vifaa kupanda, ameagiza Halmashauri kufanya tathmini ya Mwisho ya kujua ni fedha kiasi gani zinahitajika kumalisha ujenzi wa Shule hiyo ili halmashauri iweze kutenga fedha za kukamilisha.
Kadhalika, Dkt. Dugange amemshukuru Diwani wa kata ya Kiutu, Malaki Marambo na familia za jirani kwa kutoa eneo la ujenzi wa shule hiyo kutokana na kata kukoasa eneo ya kujenga.
Shule ya Sekondari ya Kiutu tayari imepokea wanafunzi wa Kidato cha kwanza 111 kati ya wanafunzi 133 waliokuwa wamepangwa kuanza masomo katika Shule hiyo.
"ARUSHA DC ni Yetu, Tushirikiane Kuijenga"
#kaziinaendelea✍✍✍✍
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.