Bilioni 1.043 Kujenga miundombinu ya Elimu Msingi na Awali (BOOST)
Milioni 40 Kujenga Miundombinu ya Sekondari (SEQUIP)
Halmashauri ya Wilaya ya Arusha Julai 1, 2025 imepokea fedha za Miradi zaidi ya Shilingi Milioni Bilioni 1 kutoka Serikali kuu kupitia Mradi wa kuboresha upatikanaji wa fursa sawa katika ujifunzaji bora wa Elimu awali na Msingi Tanzania (BOOST) na (SEQUIP)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan ameridhia fedha hiyo kiasi cha Shilingi 1,043,330,904 ,zitumike kwenye Ujenzi wa miundombinu ya shule za awali na Msingi na Milioni 40,000,000 zitumike kwenye Shule yza Sekondari Wilaya ya Arusha ili kuimarisha zaidi ujifunzaji kwa kuweka mazingira wezeshi
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Arusha Ndg Seleman Msumi ameeleza kuwa fedha hiyo itatumika kukarabati majengo Chakavu, Kujenga vyumba vya vitatu vya Madarasa na Kujenga matundu ya vyoo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha Seleman Msumi amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuiheshimisha Halmashauri ya Wilaya ya Arusha kwa kutoa fedha hiyo kuimarisha zaidi miundombinu ya Elimu na kuahidi kuisimamia kwa weledi mkubwa, ikamilike kwa wakati kwa viwango bora vinavyolingana na thamani ya fedha iliyotumika ili ianze kutoa huduma bila kuathiri Mipango na malengo ya Serikali.
Nae Afisa Mipango na uratibu Halmashauri ya Wilaya ya Arusha Bi Anna Urio ametoa rai kwa wakandarasi, Wazabuni na wananchi kufanyakazi kwa ushirikiano ili kukamilisha Miradi hii kwa manufaa ya Jamii yetu kwani uwekezaji Mkubwa unaofanywa na Serikali yetu katika Sekta ya Elimu tunapaswa kuunga Mkono kwa vitendo.
Halmashauri ya Wilaya ya Arusha ina jumla ya shule za Msingi 102 na kukamilika kwa Ujenzi na Miundo Mbinu shule ya Msingi itaongeza Hamasa ya kufanya kazi Kwa waalimu na Wanafunzi.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.