Shirika lisilo la kiserikali la DSW limeendelea kuungana na serikali na watanzania wote, kwenye mapambano ya ugonjwa hatari wa Corona unaosababishwa na virus vya Covid 19, ambalo ni tishio kwa afya na maisha ya watanzania na watu duniani kote.
Akizungumza wakati wa kupokea msaada huo, mara baada ya kikao cha tathmini ya utekeleza wa mradi wa vijana, unaotekelezwa na shirika la DSW, kilichofanyika kwenye ukumbi wa Mwenyekiti, halmashauri ya Arusha, Afisa Vijana mkoa wa Arusha , Kurwa .....licha ya kulishukuru shirika hilo kwa msaada huo, amewataka watumishi kuendelea kutoa elimu kwa jamii, hasa ya kubadili tabia na kuona umuhimu wa kunawa mikono kila wakati kwa kujikinga na gonjwa la Corona.
Amewataka wananchi kuendelea kuchapa kazi, huku wakichukua tahadhari ya kupata maambukizi ya ugonjwa wa Corona, kwa kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni, kuvaa barakoa na kuzingatia maelekezo yanayotolewa na watalamu wa afya.
Akikabidhi msaada huo, mkurugenzi wa shirika la DSW,Peter Owaga, amesema kuwa, shirika lao limeona umuhimu wa kutoa vifaa vitakavyowezesha wananchi na watumishi kujikinga na Corona kufuatia maelekezo yanayotolewa na Serikali kupitia Wazara ya Afya.
Owaga amefafanua kuwa, wametoa ndoo za kunawia mikono 22, ili wananchi katika kata za ene waweze kunawa mikono wanapofika kwenye ofisi za serikali kupata huduma kwa kuwa, tahadhari inatakiwa kufanyika muda wote.
Amefafanua kuwa, kati ya ndoo hizo 22, kwenye kata 4 za eneo linalotekelezwa mradi na shirika hilo na zitatumika kwenye ofisi za kata hizo, ndoo 7 zitumike kwenye vikundi, ndoo 5 ofisi ya vijana mkoa na ndoo 6 kwa ajili ya ofisi za makao makuu, halmashauri ya Arusha.
Hata hivyo, mkurugenzi huyo, amewasisitiza wananchi kutekeleza majukumu yao ya kijamii, huku wakichukua tahadhari ya kujikinga na ugonjwa wa Corona kwa kunawa mikono kila mara, kuvaa barakoa, kutumia vitakasa mikono.
"Ugonjwa wa Corona upo,na maisha yanatakiwa kuendelea hivyo ni vyema wananchi tuendelee kuchapakazi huku tukichukua tahadhsri ya kupata maambukizi ya ugonjwa huo, kwa kunawa mikono kwa maji na sabuni, na kufuata maelekezo yanayotolewa na Serikali na watalamu wa afya"amesisitiza mkurugenzi Owaga
Naye Afisa Maendeleo ya Jamii, halmashauri ya Arusha Angela Mvaa, amelipongeza shirika la DSW kwa kuwa wadau wa maendeleo katika halmashauri hiyo, na kuona umuhimu wa kutoa vifaa vya kunawia mikono, jambo ambalo litasaidi wananchi kujikinga na ugonjwa wa Corona.
Shilika la DSW ni mdau mkuwa wa maendeleo kwenye halmashauri ya Arusha, katika kipambana na adui, ujinga, umaskini na maradhi, kwa kuwezesha wananchi kujikwamua kifkra, kijamii na kiuchumi, kuelekea uchumi wa kati.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.