JE UNAFAHAMU KIBALI CHA UJENZI???
Kibali cha ujenzi ni Moja ya kanuni muhimu sana ya upangaji wa miji nchini Tanzania. Kila anayetaka kujenga nyumba anapaswa kufuata kanuni za ujenzi katika kibali cha ujenzi atakachopewa, mara nyingi kwa mujibu wa Sheria kibali cha ujenzi hutolewa na Mamlaka za Serikali ambazo ni halmashauri kupitia Idara ya Ardhi na Mipango Miji, Idara ya Ujenzi na Idara ya Mazingira.
UTARATIBU WA UTOAJI WA VIBALI VYA UJENZI
Kibali cha Ujenzi ni kibali kinachotolewa na Halmashauri chini ya Sheria ndogo za Udhibiti wa ujenzi holela mijini na ambacho kitamruhusu mwananchi afanye ujenzi au ukarabati wa jengo.
UMUHIMU WA KUPATA KIBALI CHA UJENZI
- Kutimiza matakwa ya kanuni za ujenzi mijini
- Kuwezesha kujenga majengo na nyumba kama yalivyoelekezwa katika mipango miji ya sehemu husika
-Kudhibiti ujenzi holela
TARATIBU & KANUNI ZA UTOAJI WA VIBALI VYA UJENZI
Kuwasilisha michoro iliyokamilika na kujaza fomu inayotolewa na Halmashauri. Report submitted for Approval (RPA)”. Fomu hii imegawanyika katika sehemu tano (5), zinazohusisha wataalamu wafuatao;
Kuwasilisha michoro iliyokamilika na kujaza fomu inayotolewa na Halmashauri Fomu itaambatanishwa na michoro iliyokamilika yaani “Architectural & Structural Drawings” na kupita kwa wataalamu wote watano (5) kama ilivyoonyeshwa hapo juu kwa ajili ya uhakiki kama ifuatavyo.
Kama michoro na nyaraka za umiliki zimekidhi vigezo zitawasilishwa kwenye kamati ya mipango miji na utoaji vibali vya ujenzi.
Baada ya michoro na nyaraka kupita katika kamati ya mipango miji na utoaji vibali itapigiwa makadirio na mwombaji atapaswa kulipia gharama husika kwenye akaunti ya Halmashauri atakayopewa.
Mwombaji ataandaliwa kibali cha ujenzi kinachosainiwa na Mhandisi wa Ujenzi na Afisa Mipango Miji wa Halmashauri.
MUDA WA UPATIKANAJI WA KIBALI CHA UJENZI
WAJIBU WA MWANANCHI
TAHADHARI
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.