FUNGUZI WA MAFUNZO YA SIKU 2 YA MFUMO WA ANWANI ZA MAKAZI KWA WENYEVITI WA VIJIJI, WATENDAJI WA KATA NA VIJIJI
Katibu Tawala Wilaya ya Arumeru Joseph Pascal Mabiti amewataka Wenyenyeviti wa Vijiji ,Watendaji wa kata na Vijiji kuhakikisha wanafanikisha uandikishaji wa Anwani za Makazi.
Ametoa kauli hiyo Katika Ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo kuhusu Mfumo wa Anwani za Makazi Kwa wenyeviti na Watendaji wa kata na Vijiji wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha, kuwataka kusimamia kwa weledi pamoja na Kutoa Elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa Anwani za Makazi.
"Kumekuwa na tabia ya baadhi ya wananchi kuharibu nguzo za majina barabara,Natoa rai kwa yeyote anayejihusisha na vitendo hivyo kuacha mara moja na sisi kama Serikali hatutasita kuwachukulia Hatua Kali za Kisheria
Aidha, Katibu Tawala Joseph Pascal Mabiti amesema kuwa Anwani ya makazi ni hitaji la msingi katika kuwezesha ukuaji wa sekta mbalimbali za kijamii na kiuchumi na ni Nyenzo muhimu ya ukuaji wa uchumi wa kidijitali ambao ndio umeshika kasi katika ulimwengu wa sasa.
" Hali hii inapelekea ongezeko kubwa la upimaji wa maeneo na ujenzi wa makazi mapya ambayo yanahitaji kutambuliwa na kupatiwa Anwani za Makazi pamoja na Kasi ya ukuaji wa Halmashauri yetu inapaswa kwenda sambamba na kasi ya utambuzi na utoaji wa Anwani za Makazi". Amesema
"sisi tutakaopatiwa mafunzo tufahamu kwamba tunahitaji kwenda kuongeza kasi ya utoaji wa Anwani za Makazi". Ameongeza
Kwa upande wake Mratibu wa Anwani za Makazi Bw. Lothy Zacharia amesema Matarajio ya Halmashauri ya Wilaya ya Arusha mi kuona kuwa Halmashauri inakuwa Mfano Bora katika utekelezaji na matumizi ya Anwani za Makazi na kuwa chachu kwa Halmashauri nyingine kuja Arusha DC kujifunza namna ya kufanikisha utekelezaji wa Mfumo wa Anwani za Makazi.
Mafunzo ya kuwajengea uwezo wenyeviti na Watendaji wa kata na Vijiji wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha kuhusu Anwani za Makazi yameandaliwa na wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwa Lengo la kuhakikisha kila mwananchi anatambulika kwa kutumia Anwani ya Makazi ili kuboresha mfumo wa maisha ya Watanzania na kuimarisha ufikishaji wa huduma
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.