Halmashauri ya Wilaya ya Arusha inategemea kupokea msaada wa magari matano kutoka kwa Kikundi cha 'Friend of German' la nchini Ujerumani kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali la Help for Maasai Children la nchini Tanzania mapema mwishoni mwa mwezi huu wa Oktoba.
Akizungumza kwa njia ya simu, Mratibu wa Mradi wa shirika hilo ndugu Harld Ppeiffer , ameyataja magari hayo kuwa ni pamoja na magari mawili ya kisasa kwa ajili ya huduma za haraka kwa wagonjwa wa dharura 'Ambulance' na magari matatu aina ya Nissani kwa ajili ya kurahisisha usafiri kwa watalamu kufika kwenye maeneo ya wananchi wakati wa kutoa huduma.
Hata hivyo katika hali ya kipekee zaidi, Ppeiffer amesema kuwa, Shirika hilo limeamua kuleta magari hayo, kwa kuyaendesha kutoka nchini Ujerumani mpaka nchini Tanzania, hususani kwenye ardhi ya Halmashauri ya Arusha huku safari yao ikiwa tayari imeanza tangu tarehe 23.09.2028 na kutarajiwa kukamilika tarehe 17.10.2018.
Amefafanua kuwa, kupitia safari hiyo ya kuleta magari hayo, itakayochukua takribani siku kumi na nne, wadau hao wanategemea kukusanya fedha kiasi cha 'Euro 300,000, fedha ambazo zitakazotumika kwenye ujenzi wa Zahanati ya Oldonyowas iliyopo kata ya Oldonyowas na kiasi kingine kutumika katika shughuli nyingine za Idara ya Afya.
Naye Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha Dkt, Wilson Mahera, amethibitisha ujio wa magari hayo kutoka shirika hilo na kusema kuwa, licha ya kulishukuru shirika hilo na serikali ya Ujerumani lakini pia magari hayo yamekuja wakati muafaka kwa kuwa halmashauri ilikuwa inakabiliwa na upungufu wa magari, ulikuwa kwa namna moja au nyingine ulikwamisha utekelezaji wa majukumu kiutendaji.
Amefafanua kuwa, magari manne kati ya hayo matano yatakabidhiwa kwa halmashauri ikiwa ni Nissan mbili na Ambulance mbili, magari yatakayotumika na Idara ya Afya kwa kutoa huduma za afya kwa wananchi huku gari moja aina ya Nissan litatumiwa na shirika hilo la Help fo Maasai Children kwa ajili ya kusimamia hiyo miradi wanayoitekeleza ndani ya Halmashauri.
Awali halmashauri ya Arusha imekuwa na uhusiano wa kirafiki na marafiki hao waishio Ujerumani,uhusiano ambao umeleta mafanikio makubwa ambayo, marafiki hao kuamua kuwasaidia wananchi wa Halmashauri hiyo kwenye sekta ya Elimu, Afya na Maji kwa kupitia shirika la 'Help for Masaai Children'.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.