• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

HALMASHAURI YA WILAYA YA ARUSHA YAZINDUA MASHINDANO YA UMISSETA NGAZI YA WILAYA ILI KUPATA TIMU ZA KUSHIRIKI NGAZI YA MKOA

Posted on: May 10th, 2025

HALMASHAURI YA WILAYA YA ARUSHA YAZINDUA MASHINDANO YA UMISSETA NGAZI YA WILAYA ILI KUPATA TIMU ZA KUSHIRIKI NGAZI YA MKOA


Katika juhudi za kuibua na kukuza vipaji vya michezo kwa vijana wa shule za sekondari, Halmashauri ya Wilaya ya Arusha imezindua rasmi mashindano ya Umoja wa Michezo wa Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA) yaliyofanyika leo 09 Mei, 2025 katika viwanja vya Shule ya Sekondari Ilboru.

Uzinduzi huo ulifanywa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha ambaye pia ni Afisa Elimu Sekondari na mlezi wa michezo wa Halmashauri hiyo, Menard Lupenza, ambapo alisisitiza kuwa mashindano hayo ni jukwaa muhimu la kuwapata wachezaji bora wapatao 120 watakaoiwakilisha Halmashauri hiyo katika ngazi ya Mkoa.

"Mashindano haya yamepitia hatua mbalimbali kuanzia ngazi ya shule hadi kata, na sasa tunashuhudia hatua ya Wilaya ambayo itatupatia kikosi cha Halmashauri ya Arusha kitakachoshiriki UMISSETA 2025 kwenye mashindano ya kimkoa," alisema Lupenza.


Aliainisha michezo inayoshindaniwa kuwa ni riadha, mpira wa miguu, mpira wa pete, mpira wa kikapu na kurusha mkuki.

Kwa upande wake, Afisa Michezo wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha, Priscus Silayo, alibainisha kuwa mashindano hayo yanajumuisha kanda nne za Halmashauri hiyo ambazo ni: Mlangarini, Kisongo, Ilboru na Ngaramtoni.

Lupenza pia alitumia fursa hiyo kuwapongeza walimu wa michezo, wataalamu, na wote waliowezesha vijana kufika hatua hiyo muhimu. Alisisitiza kuwa michezo si burudani tu, bali ni njia muhimu ya kuwaepusha watoto na vishawishi mbalimbali vinavyowakumba katika jamii ya sasa.

"Vijana wetu wapo tayari kushindana. Wameiva kisawasawa, na tunatarajia timu imara itakayoleta heshima kwa Halmashauri yetu katika mashindano ya mkoa," aliongeza.

Viongozi wote wa Halmashauri, waalimu, wakufunzi, wanafunzi na wanamichezo walionyesha mshikamano mkubwa na ari ya juu ya kushiriki, hali iliyotia matumaini makubwa kwa mustakabali wa michezo wilayani humo.


Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.