Posted On: October 10th, 2023
Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi, anatoa pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu HHassn kwa kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa (Honoris Causa) na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru Profesa Santishree Dhulipudi Pandit kwenye hafla iliyofanyika New Delhi nchini India tarehe 10 Oktoba, 2023.
Mhe. Rais Dkt. Samia amekuwa ni Mwanamke wa Kwanza kutunukiwa Shahada hiyo ya Heshima na Chuo hicho nchini India.
Ifahamike kuwa mpaka sasa Viongozi wawili tu ambao wametunukiwa Shahada hiyo ya Heshima akiwemo Rais wa Urusi Mhe. Vladmir Putin pamoja na Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Japan Hayati Shinzo Abe.
Asante mama Heshima yako, ni ya watanzania wote
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.