Na Elinipa Lupembe
Katika juhudi za kutokomeza ukatili dhidi ya watoto shirika lisilo la kiserikali la House of Happiness limezindua kituo cha kulelea watoto yatima na waishio kwenye mazingira magumu lengo likiwa ni kurejesha furaha iliyopotea kwa watoto hao kutokana na kupoteza wazazi pamoja hali ngumu ya maisha.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kituo hicho kilichopo Kijiji cha Loovilukunyi, Kata ya Kisongo, Mkurugenzi wa shirika la House of Happiness, Mohamed Kassim amesema kuwa lengo la kufungua kituo hicho ni kuwapatia watoto upendo kwa kuwapa malezi bora yatakayowarejeshea furaha na matumaini ambayo waliyapoteza kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wao.
Tunafahamu nchi yetu inakabiliwa na changamoto ya Watoto kuishi kwenye mazingira magumu kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kupoteza wazazi kunakosababisha Watoto kukosa haki zao za msingi, hivyo uwepo wa kituo hicho kutawawezesha watoto kupata huduma zote za msingi ikiwemo mavazi, malazi na chakula sambamba na kuwapatia elimu rasmi.
“Kila mtu anahitaji upendo, niwaombe wanajamii kushiriki kuwahudumia Watoto wenye mahitaji ili nao waishi kama Watoto wengine, kwa kuwa Watoto nao wanahitaji upendo ili kuwa na kizazi bora, ni furaha yangu kuwaona Watoto wakiwa na furaha pamoja na upendo”. Amesisitiza Kassim
Naye Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Arusha Seleman Msumi, amewashukuru wadau wote walioshiriki katika kuwezesha kituo hicho kufanya kazi, kwa kuwa kituo hicho ni muhimu kwa Watoto wa kitanzania ambao walipoteza matumaini kutokana na sababu mbambali za maisha.
“Watoto hawa walikosa fursa katika Maisha yao lakini House of Happiness limeona umuhimu wa kuwapa huduma za msingi zitakazo warejeshea furaha na matumaini waliyoyapoteza, kurudisha ya mtu iliyopotea ni kitu kikubwa sana hata mbele za Mungu”. Amesema Mkurugenzi Msumi.
Aidha wananchi wa eneo hilo wamelishukuru shikika hilo kwa kujenga kituo cha Watoto wenye uhitaji na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano ili kufikia lengo la shirika na Serikali kwa ujumla wake la kuwahudumia watoto katika jamii.
“Watoto wanahitaji upendo wakati wote, hivyo wanapokosa mahitaji yao ya msingi kama vile chakula, maladhi na mavazi ni chanzo cha cha ukatili dhdi yao. Japo kuna hali ngumu ya maisha lakini kila mzazi anapaswa kufanya wajibu wake ili kuwawezesha Watoto kutimiza ndoto zao”. Alisema Simon Mollel, Mkazi wa Kijiji cha Loovilukunyi, Kata ya Kisongo
Naye Diwani wa kata ya Kisongo Mhe. Godson Loning’o amesema kuwa uwepo wa kituo hicho ni zawadi kubwa kutoka kwa mungu kupitia kwa shirika hilo la Hose of happiness na kuitaka jamii kuangalia mazingira ya watoto wao ili kuwapatia stahiki zao kama haki ya msingi.
Hata hivyo kituo hicho ambacho ujenzi wake ulianza mwaka 2019, kimezinduliwa kikiwa na Watoto kumi na moja (11) wakike watatu (3) na wakiume nane (8) na kinategemea kuhudumia watoto sitini na nne (64) wenye umri wa kati ya miaka mitatu (3) hadi kumi na mbili(12) kutoka sehemu yoyote ndani ya Tanzania bila kujali hali zao za kiafya.
ARUSHA DC,
TUPO KAZINI.
PICHA ZA MATUKIO WAKATI WA UZINDUZI WA KITUO CHA WATOTO YATIMA NA WAISHIO KATIKA MAZINGIRA MAGUMU (HOUSE OF HAPPINESS)
Baadhi ya watoto wanaolelewa katika kituo cha House of Happiness wakiwa katika ukumbi wa kituo hicho wakati wa hafla ya uzinduzi
Mkurugenzi wa Kituo cha House of Happiness, Mohamed Kassim akifanya utambulisho wa wageni waliohudhuria katika hafla ya uzinduzi wa kituo cha watoto yatima na wale waishio katika mazingira magumu
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Arusha Seleman Msumi (kushoto) akiteta jambo na mdhamini mwenza wa kituo cha House of Happiness mara baada ya uzinduzi wa kituo hicho
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.