Na. Elinipa Lupembe.
Jamii imetakiwa kutambua umuhimu ya kinga tiba ya magonjwa ya kichocho na minyoo inayotolewa na serikali kwa watoto wa kuanzia umri wa miaka 5 mpaka 14, ikiwa na kusudi la kuwakinga na kuwatibu watoto dhidi ya magonjwa ya kichocho na minyoo tumbo, magonjwa ambayo yana athari kubwa kwa afya za watoto pamoja na kuathiri makuzi yao.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa halmashauri ya Arsuha, Mheshimia Ojung'u Salekwa wakati akizindua zoezi la siku mbili la utoaji wa vidonge vya kinga tiba dhidi ya magonjwa ya kichocho na minyoo tumbo kwa watoto wa kuanzia umri wa miaka 5 mpaka 14 katika halmashauri hiyo, uzinduzi uliofanyika shule ya msingi Naurei kata ya kiutu.
Mwenyekiti Salekwa amesema kuwa ,serikali inatambua kuwa kati ya magonjwa yanaochangia udumavu wa afya kwa watoto ni pamoja na minyoo tumbo na ugonjwa wa kichoo, magonjwa yanayotokana na mazingira wanayotumia watoto kucheza, hivyo ni vema kuzingatia kuwapatia dawa za kinga ambazo zipo na hutolewa na serikali bure.
"Wazazi na walezi mnatakiwa kuunga mkono jitihada za serikali za kuhakikisha watoto wetu wanapata kinga tiba dhidi ya kichocho na minyoo, kwa kuwa magonjwa hayo yanadumaza afya na ukuaji wa mtoto, na baadaye kumuathiri mtoto kiakiali na kisaikolojia pia"amesema Mwenyekiti huyo.
Hata hivyo Mganga Mkuu halmashauri ya Arusha, Dkt. Petro Mboya, amesema kuwa halmashauri ya Arusha, inategemea kutoa kinga tiba ya magonjwa ya minyoo na kichocho kwa jumla ya watoto 89,914 wa kuanzia miaka 5 mpaka 14, walioandikishwa shule na wale wasioandikishwa shule, zoezi hilo likifanyika kwenye shule zote za msingi 163 za halmashauri ya Arusha, ikiwemo shule 96 za serikali na shule 67 za binafsi.
Dkt. Mboya ambainisha kuwa magonjwa ya minyoo na kichocho yana madhara makubwa katika makuzi ya mtoto, kwa kuwa minyoo hufyonza chakula anachokula mtoto, na matokea yake mtoto huanza kudhoofika kiafya kutokana na lishe yote anayokula kushambuliwa na minyoo, hivyo ni vema kumkinga mtoto dhidi ya minyoo ili kuimarusha afya yake.
Hata hivyo Dkt. Mboya, aliwataka wazazi na walezi kuyapuuza maneno ya kubeza dawa hizo kuwa zina madhara kwa watoto, jambo ambalo kitaalamu si la kweli, dawa hizo ni salama na zinatibu na kukinga magonjwa hayo ya kichocho na minyoo ya tumbo, huku akifafanua kuwa ni kweli kuna baadhi ya watoto huweza kutapika au kujisiskia vibaya, jambo ambalo ni la kawaida kulingana na mwili wa mtoto, na kuyaita matokeo hayo ni maudhi madogo madogo yanayotokana na dawa na kutokuwa na madhara yoyote makubwa zaidi.
Nayr mwalimu mkuu, shule ya msingi Naurei, mwalimu Getrude Tarimo, amesema kuwa wamejiandaa vema kukamilisha zoezi hilo kwa kuhakikisha watoto wote, waliogpfika shuleni wanapatiwa kinga tiba hiyo, kwa kuzingatia maelekezo ya watalamu wa afya.
"Kabla ya kupatiwa dawa hizo, tumelekeezwa mtoto lazima awe amekula chakula na kushiba, tayari tumewapa watoto wetu chakula, huku zoezi la kugawa dawa likiendelea"amesema mwalimu Getrude
Zoezi hilo la kutoamKinga tiba ya kichoho na minyoo ni zoezi la kitaifa na hufanyika kila mwaka mara moja, lifanyika kwa muda wa siku mbili katika halamshauri ya Arusha huku jumla ya watoto 89,914 wakitegemea kupata kinga tiba hiyo.
Mwenyekiti wa halmashauri ya Arusha, mheshimiwa Ojung'u Salekwa, akimnywesha vidonge mmoja wa wanafunzi wa shule ya msingi Naurei, ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa zoezi la siku mbili la kugawa dawa za Kinga Tiba ya magonjwa ya Kichocho na minyoo tumbo kwa watoto wa miaka 5-14 katika halamshauri ya Arusha.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.