• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

JAMII IMETAKIWA KUFAHAMU KUWA, INA WAJIBU WA KUCHANGIA DAMU

Posted on: September 9th, 2020

Na. Elinipa Lupembe.

   Jamii imetakiwa kufahamu kuwa ina wajibu wa kuchangia damu na kutambua umuhimu wa kushiriki zoezi hilo ili kusaidia kuokoa maisha ya wagonjwa wanaohitaji hudumu ya damu kwa dharura ikiwemo kina mama wajawazito na watoto licha ya kuwa zoezi hilo ni la hiari.

     Rai hiyo imetolewa na mkurugenzi mtendaji, halmashauri ya Arusha, Saad Mtambule, alipokuwa akichangia damu, wakati wa zoezi maalum la uchangiaji wa damu salama, lililohusisha watumishi wa halmashauri hiyo na wageni waliofika kupata huduma katika halmashauri hiyo kwa siku hizo za zoezi hilo.

    Mkurugenzi Mtambule ameweka wazi kuwa, licha ya kuwa uchangiaji wa damu ni jambo la hiari, lakini kuna umuhimu mkubwa wa kila mtu kutambua wajibu wake wa kuchangia damu, kutokana na uhitaji mkubwa wa damu kwa wagonjwa wa dharura katika vituo vya kutolea huduma za Afya.

    "Kama tujuavyo, uhitaji wa damu ni wa dharura na kila mtu anapaswa kujua kuwa, muda wowote yeye ni muhitaji wa damu kwa dharura, hivyo tuna wajibu wa kujitolea  kuchangia damu, ili kuwa na damu ya kutosha katika benki za damu, jambo lililotusukuma kuendesha zoezi la hiari kwa watumishi wa Arusha DC, tukiwa na lengo kuokoa maisha ya wagonjwa wenye uhitaji wa damu wakati wote na kuongeza matumaini yao ya kuishi". Amesema Mkurugenzi Mtambule.

     Hata hivyo amefafanua kuwa, zoezi hilo limefanyika kutokana na uhaba wa damu kwenye benki ya damu, katika hospitali ya wilaya hiyo ya Olturumet, jambo ambalo lililosababisha kuendesha zoezi la maalumu uchangiaji damu kwa hiari kwa watumishi wa halmashauri ya Arusha, huku watumishi wakijitokeza kushiriki zoezi hilo.

     Nao watumishi wa halamshauri ya Arusha, waliojitokeza kuchangia damu katika zoezi hilo, wameupongeza  uongozi wa halamshauri hiyo kupitia mkurugenzi mtendaji kwa kuendesha zoezi hilo kwa watumishi ndani ya ofisi zao, zoezi ambalo matokeo yake yanatarajiwa kwenda kuokoa maisha ya wagonjwa hususani mama na mtoto wakati wa kujifungua.

      Afisa Uchaguzi, halmashauri ya Arusha, Hadija Mkumbwa, licha ya kuvutiwa na kushiriki zoezi la uchangiaji damu, amekir kuwa, mara nyingi watumishi wamekuwa ni wahamasishaji wa zoezi la uchangiaji damu, na sio wachangiaji damu, kupitia zoezi hilo maalumu kwa watumishi limewapa fursa ya kuwa ni sehemu ya  watu, wanakwenda kuokoa maisha ya watu wengine.

     Naye Mganga Mkuu, halmashauri ya Arusha Dkt. Petro Mboya, amewatoa hofu watu wanaoogopa kuchangia damu kuwa, kitendo hicho hakina madhara yotote kiafya kwa mchangiaji damu mwenye afya njema, na kuwataja watu watu wasiofaa kuchangia damu ni pamoja na wenye magonjwa ya kisukari, presha, watu waliofanyiwa upasuaji mkubwa karibuni na wale wanaotumia dawa za muda mfupi na mrefu kwa wakati huo.

    Aidha Dkt. Mboya amewashukuru watumishi wote waliojitokeza kuchangia damu, na kukiri zoezi hilo kwenda kwa mafanikio, huku wakiwa wamefanikiwa kukusanya kiasi cha uniti 21 za damu.

Naye Mratibu wa Damu Salama na Afisa Ustawi wa Jamii, halmashauri ya Arusha, Beatrice Tangi, amesema kuwa, zoezi la uchangaji damu ni zoezi la kitaifa ambalo limekuwa likiendelea  kila siku, jukumu lao watalamu ni kuhamasisha watu kujitoa kuchangia damu kwani hakuna kiwanda kinachoweza kutengezeza damu ya kumuongezea binadamu, bali ni binadamu pekee ndio wenye uwezo wa kuokoa maisha ya wagonjwa kwa kuchangia damu.


PICHA ZA MATUKIO YA UCHANGIAJI DAMU WATUMISHI WA ARUSHA DC








Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.