Na Elinipa Lupembe
Jamii imetakiwa kuhakikisha kuwa, wanatunza mazingira kwa kuotesha miti kwenye mazingira yanayowazunguka ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi yaliyotokana kuharibika kwa uoto wa asili.
Rai hiyo imetolewa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa 2023, ndugu Abdallah Shaib Kaim wakati akitembelea na kukagua miradi ya maendeleo.
Amesema kuwa, ukataji wa miti unasababisha uharibifu wa mazingira kwa kiasi kikubwa janga ambalo linasababisha uhaba wa mvu na ukame,mmomonyoko wa udongo.
Madhara ya uharibifu wa mazingira yanafahamika ni pamoja na ukosefu wa mvua unaosababisha ukame na jangwa, mvua zinazozidi na kusababisha mafuriko, uharibifu wa uoto wa asili na kusababisha vifo kwa viumbe hai, ni vema kila mtanzania akajitoa kutunza mazingira
"Sote tunafahamu kuwa Mazingira ni uhai, kwa kuwa uhai wa binadamu na viumbe vyote unategemea mazingira, tuoteshe miti kwa wingi, tutunze vyanzo vya maji, tusifanye shughuli za kibinadamu karibu na vyanzo vya maji, zaidi tufuge mifugo michache kwa kuzingatia ushauri wa kitaalmu" Ameweka wazi.
Ninyi ka jamii ya wafugaji fanyeni utaratibu wa kufuga kitaalamu kwa kutumia eneo dogo, sambamba na kuhifadhi maeneo ya kuotesha majiani kwa ajili ya mifugo yenu na sio kufuga holela na kuacha mifugo ikizurura, jambo hili huaribu mazingira na kusababidha mmomonyoko wa udongo kwenye maeneo yetu.
Hata hivyo kiongozi huyo ameshiriki kuotesha miti kwenye maeneo yote ya miradi ikiwa ni ishara ya utunzaji wa mazingira unaoendana na Kauli mbiu ya Mwenge wa Uhuru 2023.
Aidha Kiongozi huyo wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa, amewataka wananchi wa halmashauri ya Arusha kuendeleza kampeni hiyo ya upandaji miti kwa kuhakikisha kila mwananchi anaotesha miti yake na kuitunza mpaka inakua.
KAULI MBIU: " TUNZA MAZINGIRA, OKOA VYANZO VYA MAJI KWA USTAWI WA VIUMBE HAI KWA UCHUMI WA TAIFA"
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.