• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

JAMII YATAKIWA KUVUNJA UKIMYA KUZUNGUMZA NA VIJANA JUU YA AFYA YA UZAZI

Posted on: November 26th, 0201

Na. Elinipa Lupembe.

Jamii imetakiwa kuvunja ukimya na kuachana na mila potofu, za kudhani kumfundisha watoto masuala ya afya ya  uzazi  na uzazi wa mpango ni kumfanya aanze kujiingiza kwenye mahusiano ya kingono mapema.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha, Afisa Mipango, Anastazia Tutuba, wakati akifungua kikao kazi cha siku moja kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano halmashauri ya Arusha, kilichojumuisha wadau mtambuka wa afya ya uzai kwa vijana,  amesema kuwa usiri miongoni mwa jamii, unasababisha watoto wengi kujiingiza kwenye mahusiano ya kingono katika umri mdogo kujikuta wakipata mimba za utotoni na ndoa za utotoni,

Ameitaka jamii hasa wazazi kuvunja ukimya na kuanza kuzungumza na watoto wao, juu ya afya ya uzazi na uzazi wa mpamgo, kwa kuzingatia mabadiliko yao ya kimwili na kiakili yanayojitokeza wakati wa kukua kwa via vya uzazi, jambo litakalo wawezesha kukabiliana na mihemko ya mwili yanayotokana na mabadiliko hayo.

Vijana wengi wamejikuta wakishauriana wao kwa wao, huku wakipeana taarifa zisizo sahihi na kijiingiza kwenye mahusiano ya kimapenzi na kuanza kujamiiana katika umri mdogo bila  kufahamu madhara ya matokeo ya vitendo hivyo na kusababisha mimba zisizotarajiwa na ndoa za utotoni, huku vijana hao wakikatiza masomo na kushindwa kufikia malengo yao ya kimaisha.

Serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali yameweka mipango mingi ya maendeleo kwa jamii na taifa, wazazi na jamii isipokua makini, itakipoteza kizazi hiki na kushindwa kuendeleza mipango mizuri iinayoandaliwa na serikali sasa.


" Tuungane kuwafundisha vijana wetu masuala ya afya ya uzazi na uzazi wa mpango kwa vijana, ili kuwa na kizazi chenye kujitambua na kutambua majukumu yao binafsi na ya taifa na si kuwa na vijana wenye msongo wa mawazo kutokana na kujeruhiwa na mahusino, yanayokatiza ndoto zao" amesema Tutuba

Hata hivyo, mratibu wa mradi shirika la JHIPEIGO, Arusha,  Waziri Njau, amefafanua kuwa suala la afya uzazi na uzazi wa mpango kwa vijana ni jukumu la kila mtu, kuwa karibu na watoto, kuzungumza nao na kuwaelekeza kwenye vituo vya kutolea huduma za afya kukutana na watalamu wa afya kwa ushauri nasaha, kutasaidia vijana kufikia ndoto zao.


Aidha amewataka walimu wa afya shuleni, licha ya kuwafundisha masomo mengine wapate nafasi ya kuanzisha klabu za afya, ili kuwajengea vijana uwezo wa kujitambua na kutambua afya ya uzazi inayoendana na mabadiliko yao kimwili, kiakili na kisaikolojia sambamba na jinsi ya kukabiliana na changamoto za mabadiliko hayo.


Naye Afisa Vijana halmashauri ya Arusha, Ahadi Mlai amethibitisha kuwa, uelewa mdogo wa jamii juu ya afya ya uzazi kwa vijana, imekua ni changamoto inayokatiza ndoto za vijana wengi na kuitaka jamii kushirikiana kuwaelimisha watoto juu ya afya ya uzazi, na kuwasihi vijana kufika kwenye vituo vya afya kupata taarifa sahihi za afya ya uzazi kupitia Huduma Rafiki kwa Vijana zinazotolewa kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya

Amesema kuwa kikao kazi hicho kimewakutanisha wadau wa afya ngazi ya halmashauri, maafisa watendaji wa kata, walimu wa afya shuleni, viongozi wa dini na jamii, lengo likiwa kuwa na uelewa wa pamoja juu ya afya ya uzazi na uzazi wa mpango kwa vijana, na wao kuhamasisha jamii kutambua umuhimu wa huduma hiyo kwa vijana.

Halmashauri ya Arusha kwa kushirikiana na shirika la JHPIEGO Tanzania, wanatekeleza mradi wa Tupange pamoja na Huduma Rafikoi kwa vijana, mradi unaofadhiliwa na Bill &Melinda Geti wa nchini Marekani.

Awali jumla ya vituo vya afya 15 vya halmashauri ya Arusha,vinatoa huduma Rafiki kwa Vijana, shime vijana tusione aibu, tukapate huduma ya afya ya uzazi, huduma zinatolewa bure na kwa usiri.





Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.