JUKWAA LA MWAKA LA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI
Arusha DC
Halmashauri ya Arusha Wilaya ya Arumeru, kupitia idara ya maendeleo ya jamii kushirikiana na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali (NGO), imeandaa jukwaa la mwaka la Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali ambalo limefanyika katika Ukumbi wa Mikutano ya Halmashauri ya Arusha wilayani Arumeru.
Akifungua kikao hicho Bi. Elizabeth Ngobei afisa rasimali watu Halmshauri ya Arusha kwa niaba ya Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo ndugu Sulemani Msumi, Ngobei amesema lengo la jukwaa hilo ni kujengeana uwezo yaani “capacity building” na uelewa wa pamoja kuhusu taratibu za usimamizi wa Mashirika hayo, vilevile kujadili mchango wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali katika maendeleo ya Taifa, ili kuweza kubainisha namna shughuli za Mashirika hayo zinavyoweza kwenda sambamba na mipango ya kitaifa, ikiwa ni pamoja na kuimarisha uhusiano baina ya Serikali na Mashirika hayo.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.