Na Elinipa Lupembe.
Jumla ya Wanafunzi 4,999, wavulana 2,106 na wasichana 2,893 halmashauri ya Arusha wanategemea kufanya mtihani kwa Taifa wa kuhitimu Kidato cha 4 unaonza tarehe 14, Novemba 2022 kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA).
Mkurugenzi Mtendaji na Mwenyekiti wa Kamati ya Mitihani halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi, amebainisha kuwa idadi hiyo ya watahiniwa inajumuisha watahiniwa wa shule (school candidates), watahiniwa wa kujitegemea (private Candidates) pamoja na watahini wa Maarifa (QT).
Ameeleza kuwa, tayari maandalizi yote yamefanyika kwa mujibu wa taratibu za Mitihani ya Taifa huku wanafunzi na walimuawasimamizi wameshapewa mafunzo ya usimamizi wa mtihani huo.
Aidha amewataka wasimamizi wa mitihani, kuzingatia kanuni, sheria na taratibu wakati wotewa mitihani na kutokujiingiza kwenye aina yoyote ya vitendo vya udanganyifu kwa kuwa, lemgo la mitihani hiyo ni kuwapima wanafunzi kulingana na kile walichojifunza kwa miaka yote 4.
"Niwatake watalamu wote wanaohusika na usimamizi wa mitihani, kujiepusha na vitendo vilivyo kinyume na maadili ya mitihani, hakikisheni mnawasimamia wanafunzi hao kwa uaminifu ili waweze kufikia ndoto zao na sio kuwaingiza kwenye matatizo yasiyo ya lazima". Amesisitiza Mkurugenzi Msumi
Hata hivyo Mkuu wa shule ya sekondari Oldonyosmabu, Mwl. Loshai Moita, amesema kuwa walimu wamewaandaa wanafunzi vema kisaikolojia na kiakili, wamejengewa uwezo wa kujiamini wakati wote wa mitihani kwa kuwa mtihani huo ni sawa na mitihani mingine ambayo huifanya mara kwa mara.
"Tumewafundisha wanafunzi wetu na kumaliza mada zote, tumewapa majaribio na mitihani ya kutosha, tumewaandaa kisaikolojia pia, kazi iliyobaki ni kwao, ila tunaamini hatutakuwa na divission 0 hata moja" .Amebainisha Mkuu huyo wa shule.
Awali Mkuu wa Idara ya Elimu sekondari, halmashauri ya Arusha, Mwl. Menard Lupenza amefafanua kuwa kati ya watahiniwa 4,999 wanaofanya mitihani mwaka 2022, watahiniwa wa Shule ni 4,658 wavulana 1,950 na wasichana 2,708, watahiniwa wa Kujitegemea ni 307 wavulana 134 na wasichana 167 huku watahiniwa wa Maarifa ni 40 wavulana 22 na wasichana 18.
Uongozi wa Halmashauri ya Arusha, unawatakia kila la kheri watahiniwa wote, wanaofanya mtihani wa kidato cha 4 mwaka 2022, unaoanza tarehe 14, Novemba 2022.
MWENYENZI MUNGU AWASIMAMIE!!!!
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.