KAIMU MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA ARUSHA BI.NGOBEI AUTAKA UONGOZI WA SHULE YA SEKONDARI LIKAMBA KUONDOA SIFURI KATIKA MATOKEO YA MITIHANI YA KITAIFA.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha, Bi. Elizabeth Ngobei ameutaka Uongozi wa Shule ya Sekondari Likamba kuongeza juhudi katika ufundishaji ili kuongeza ufaulu kwenye mitihani ya Kitaifa na kuondoa ufaulu hafifu kwa wanafunzi.
Bi.Ngobei ambaye alikuwa mgeni rasmi ameyasema hayo wakati akiongea na wazazi, Walimu na wanafunzi wakati wa Mahafali ya kwanza ya kidato cha nne katika shule hiyo yaliyofanyika tarehe 17/11/2024.
" Tunatambua kabla ya Mtihani wa Taifa wa kidato cha nne huwa wanafunzi mnafanya mitihani ya majaribio kwa lengo la kupima uelewa wenu darasani,,hivyo nitumie nafasi hii kuwasihi waalimu kuondoa ufaulu hafifu mliuona kwenye mitihani hiyo ya majiribio ili kuwawezesha Wanafunzi kupanda kiufaulu katika mitihani yao ya mwisho. Alisema Ngobei
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.