Wajumbe wa bodi mpya ya Mamlaka ya Maji Ngaramtoni (NGAUWSA) wametakiwa kuweka mikakati thabiti ya kupatikana kwa lita milioni 4.2 za maji, zinazotakiwa kutumika kwa siku moja na wakazi wa Mamlaka ya Mji mdogo Ngaramtoni.
Wajumbe hao wametakiwa kutafuta lita hizo za maji kufuatia Mamlaka ya Maji NGAUWSA kuzaliza maji kiasi cha lita milioni 2.8 kwa siku, huku mahitaji ya maji kwa siku moja kwa wakazi wa eneo hilo ni lita milioni 7.
Kufuatia uzalishaji huo wa chini ya kiwango cha uhitaji wa maji kwa jamii, kumesababisha changamoto kubwa ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi hao.
Akizungumza wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa mpya Bodi ya NGAUWSA, mgeni rasmi Kaimu mkuu wa wilaya ya Arumeru, mhe. Idd Kimanta amesema kuwa, kazi kubwa ya Bodi ya NGAUWSA ni kuweka mikakati thabiti ya kutafuta namna ya kupata lita milioni 4.2 iki kufikia lita milioni 7 zinazohitajika na wakazi wa Ngaramtoni kwa siku.
Wajumbe hao wametakiwa kutafuta lita hizo za maji, kufuatia Mamlaka ya Maji Ngaramtoni kuzalisha maji lita milioni 2.8 kwa siku, huku mahitaji ya maji kwa siku moja ni lita milioni 7.
Kufuatia uzalishaji huo wa chini ya kiwango chabuhitaji wa maji kwa jamii, kumesababisha changamoto kubwa ya upatikanaji wa huduma ya maji kwa wananchi hao.
Akizungumza wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa mpya Bodi ya NGAUWSA, mgeni rasmi Kaimu mkuu wa wilaya ya Arumeru, mhe. Idd Kimanta amesema kuwa, kazi kubwa ya Bodi ya NGAUWSA ni kuweka mikakati thabiti ya kutafuta namna ya kupata lita milioni 4.2 iki kufikia lita milioni 7 zinazohitajika na wakazi wa Ngaramtoni kwa siku.
Ameongeza kuwa baada ya NGAUWSA kuanzishwa mwaka 2015 imefanikiwa kutoa huduma ya maji kwa asilimia 40% tu, huduma ambayo haiwafikia hata nusu ya wakazi, huku wakipambana kufikia mpango wa serikali wa kufikia asilimia 95% ya upatikanaji wa maji mijini ifikapo 2010.
"Ndugu zangu wajumbe wa bodi hii ya NGAUWSA mnakazi kubwa ya kufanya,ya kuhakikisha asilimia 50% zinapatikana ili kufikia lengo la serikali la asilimia 95% ifikapo mwaka 2020 pamoja na kutafuta lita milioni 4.2. ili kufikia lita milioni 7 zinazohitajika kwa siku na wananchi wenu" amesema Kimanta.
Aidha amewaasa wajumbe hao wa bodi kutambua kuwa, ili huduma ya maji iweze kupatikana na kufikia malengo, bodi ina jukumu la kutoa huduma za maji na kuifanya NGAUWSA kujiendesha kibiashara, kwa kuhakikisha watu wanalipia maji na kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato.
Mheshimiwa Kimanta hakusita kuwashauri kuwa ili kufikia malengo ni vema kutumia changamoto ya huduma za maji kwa wananchi wa mamlaka ya mji mdogo Ngaramtoni na zile zinazoikabili mamlaka ya maji NGAUWSA zigeuzwe kuwa fursa.
Awali Kaimu mkuu wa wilaya Kimanta, amemkabidhi kila mjumbe begi lenye vitabu venye miongozo na majukumu ya bodi, na kusema kuwa amewakabidhi silaha za kuhakikisha usalama wa afya za wananchi wao, kwa kuwapatia huduma ya maji safi na salama, ambayo ni kinga ya magonjwa ya mlipuko.
Naye Mwenyekiti wa Mamlaka ya mji mdogo Ngaramtoni mhe. Elias Munisi amesema wajumbe wote wa mamlaka wako tayari kutoa ushirikiano kwa Bodi hiyo ili kuhakikisha maji safi na salama yanapatikana kwa wananchi wote wa Mamlaka bila kujali tofauti za kitikadi.
Hata hivyo meneja wa NGAUWSA, Clayson Kimaro amesema kuwa, wanamatarajio makubwa ya kupatikana kwa lita zaidi ya milioni 3 kwa siku ifikapo mwishoni mwa mwaka huu 2018, baada ya mradi wa maji Ngaramtoni ulio katika hatua za mwisho na mradi wa maji wa vijiji vitano ulio katika hatua za awali, unaotegemea kukamilika mwezi Novemba, 2018.
Kimaro ameendelea kufafanua kuwa, kukamilika kwa miradi hiyo, kutaongeza usambazaji wa maji kwa wateja katika eneo la Mamlaka ya Mji mdogo Ngaramtoni.
Mwenyekiti wa Bodi ya NGAUWSA, John Sirikwa amesema kuwa, licha ya Changamoto zinazoikabili mamlaka hiyo, wao kama wajumbe wa Bodi wamejipanga kushirikiana na viongozi, watalamu na wananchi ili kuhakikisha huduma ya maji inapatikana kwa asilimia 95% ifikapo mwaka 2020 kama agizo la serikali ya awamu ya tano linavyotaka.
Sirikwa Amesema kuwa wamechukua ushauri wa mkuu wa wilaya wa kugeuza changamoto zote kuwa fursa, na kuifanya NGAUWSA kuwa mamlaka ya kutoa huduma kwa wananchi yenye mikakati thabiti ya kibiashara.
Bodi ya mamlaka ya maji NGAUWSA imezinduliwa leo ikiwa na jumla ya wajumbe saba, baada ya mamlaka hiyo kusajiliwa na wajumbe wake kupatiwa mafunzo yenye lengo la kuwajengea uwezo juu ya majukumu yao katika uendeshaji na Mamlaka hiyo ya maji.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.