Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Idd Kimanta ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Monduli amepokea msaada wa madawati 740 kwa shule 13 za Wilaya ya Arumeru zinazozunguka shamba hilo kwa lengo la kutatua changamoto ya upungufu wa madawati unaozikabili shule hizo.
Madawati hayo yametolewa na Uongozi wa Shamba la Miti la Msitu wa Meru-Usa ikiwa ni mchango wa shmba hilo kwa jamii inayozunguka shamba hilo na kuunga mkono juhudi za serikali za kuhakikisha shule zina madawati ya kutosha kutokana na ongezeko kubwa la wanafunzi kwa sasa.
Akizungumza wakati wa kukabidhi madawati hayo meneja wa Shamba Robert Faustine amesema kuwa wameamua kutoa madawati kwa shule hizo kwa kuwa zinaupungufu mkubwa wa madawati ukilinganisha na idadi ya wanafunzi na baadhi ya shule hizo kuwa ni mpya.
Ameongeza kuwa ofisi inatambua upungufu wa madawati kwenye baadhi ya shule zinazozunguka shamba hivyo itaendelea kushirikiana na taasisi binafsi kutatua tatizo hilo.
Hata hivyo Faustine amesema kuwa kati ya shule hizo 13 kila shule imepata madawati 56 na kuzitaja shule hizo ni pamoja na shule ya msingi Lemong'o, Ngedeko, Lesakata Farm, Olmotonyi, Oldonyowas, Sambasha na Olkokola za Halmashauri ya Arusha na shule za Urisho, Sangananu, Ngongongare na Sakila za Halmashauri ya Meru.
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Arumeru ameshukuru kwa msaada huo na kuwataka walimu kahakikisha wanasimamia vema utunzaji wa madawati hayo pamoja kufundisha kwa bidii na kuongeza kiwango cha ufaulu.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.