Na.Eliniapa Lupembe.
Wajumbe wa Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango, halmashauri ya Arusha, wamefanya ziara ya kukagua miradi 6 ya maendeleo inayotekelezwa katika halmashauri hiyo, kufuatika sheria, kanuni na taratibu za serikali za mitaa, inayoitaka Kamati hiyo ya Fedha kukagua miradi kila baada ya miezi mitatu katika mwaka wa fedha husika.
Katika ziara hiyo wajumbe hao, wameridhishwa na utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa, yenye thamani ya shilingi milioni 326.4 katika sekta ya elimu, afya na utawala, miradi iliyotekelezwa kupitia fedha za serikali kuu, wadau wa maendeleo ktoka sekta binafsi, halmashauri, pamoja na miradi inayotekelezwa kwa nguvu za wananchi, huku wakiweka wazi kuriidhishwa na thamani ya miradi kwa kulinganisha na fedha zilizotumika.
Wajumbe hao wa Kamati ya fedha, licha ya kuridhishwa na utekelezaji wa miradi hiyo, wamepongeza juhudi za wananchi na wadau wanaochangia utekelezaji wa miradi hiyo, pamoja na kuweka mikakati thabiti ya kutatua changamoto zinazojitokeza kwenye sekta ya elimu, afya na maji na utawala, changamoto zilizojitokeza kwenye maeneo yaliyotembelewa, lengo likiwa ni kuendelea kuboresha na kurahisisha upatikanaiji wa huduma muhimu kwa wananchi wa halmashauri hiyo.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango na Mwenyekiti wa halmashauri ya Arusha, Mhe. Ojung'u Salekwa, amewapongeza watalamu wa halmashauri hiyo, kwa utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo na kuwataka kuendelea kutatua changamoto zinazojitokeza kwenye maeneo yote, lengo likiwa kuboresha hali ya upatikanaji wa huduma kwa wananchi wa halmashauri.
Naye Afisa Mipango halmshauri ya Arusha, Anna Urio, ameitaja miradi liyotembelewa na Kamati hiyo ni pamoja na miradi ya ujenzi wa vyumba 3 vya madarasa, shule ya msingi Ilkiding'a vyenye thamani ya shilingi milioni 60, fedha kutoka Mamlaka ya Elimu Tanzania - TEA, mradi wa miundombinu ya shule ya sekondari Oldonyowas yenye thamani ya shilingi milioni 165, ikijumuisha ujenzi wa vyumba vya 3 vya madarasa, nyumba mbili za walimu zenye sehemu mbili (2 in 1), vyoo pamoja na ujenzi wa maabara ya masomo ya Sayansi, ujenzi unaotekelezwa kwa nguvu za wanachi unaokadiriwa kugharimu shilingi milioni 56 ukiwa katika hatua za awali.
Ameendela kueleza kuwa, wajumbe hao walitembelea, mradi inayotekelezwa kwa ufadhili wa wadau wa maendeleo, iliyojumisha ujenzi wa bwalo la chakula shule ya msingi Ilboru, kitengo cha elimu maalumu, mradi unaotekelezwa kwa ufadhili wa shirika la Abercrombie &Kent, utakaogharimu kiasi vha shilingi milioni 54, pamoja na ujenzi wa jengo la mama na mtoto, jengo la maabara katika zahanati ya Mlangarini, majengo yanayojengwa kwa ufadhili wa shirika la Rizkwaan Ltd kwa gharama ya shilingi milioni 56.7.
Hata hiyo kamati hiyo ilifanikiwa kutembelea maeneo mawili yanayomilikiwa na halamshauri ya Arusha, yaliyoko eneo la Burka Jiji la Arusha, maeneo ambayo yametengwa maalum na halmashauri hiyo kwa ajaili ya uwekezaji kwa kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati ikiwa ni eneo la mradi wa michezo lenye ukubwa wa eka 8, pamoja na eneo la soko lenye ukubwa wa Heka 1.5, pamoja na eneo la uwekezaji la Engira Road nalo likiwa eneo la Jiji la Arusha.
Awali kamati ya Fedha, Utawala na Mipango, hufanya ziara ya kukagua utekelezaji wa shughuli za miradi ya maendeleo, na kufanya tathmini kwa kuweka maazimio na baadaye kufuatiwa na kikao cha kamati hiyo waa robo husika, kwa kipindi cha miezi mitatu ya mwaka wa fedha, na baadaye kuwasilishwa kwenye mkuatano wa Baraza la Madiwani.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.