Wajumbe wa Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango, wametembelea na kukagua mradi wa ukarabati wa kituo cha walimu (TRC) Mringa, ujenzi uliogharimu kiasi cha shilingi milioni 22 fedha kutoka OR - TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia mradi wa (GPE -LANES II)
Akisoma taarifa ya utejelezaji wa mradi huo Afisa Elimu Kata ya Oloirien Mwl. Digna Swai, amesema kuwa, kiasi hicho cha fedha kimetumika kukarabati jengo hilo pamoja na kunua samani za ndani.
Hata hivyo wajumbe wa Kamati hiyo ya fedha, wapongeza usimamizi mzuri wa ukarabati wa kituo hicho cha walimu, kituo ambacho kitawapa walimu fursa ya kutoa mafunzo wawapo kazini.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Arusha, Mhe. Dkt. Ojjunng'u Salekwa, amethibitisha uzuri na ubora wa kazi iliyofanyika na kutoa pongezi na shukrani kwa wataalam wote, waheshimiwa madiwani waliohusika katika usimamizi wa ukarabati wa kituo hicho
Naye Diwani kata ya Olturoto, Mhe. Baraka amethibitisha kuwa kazi iliyofanyika ni nzuri na inaonekana hata kwa macho ya kawaida kwamba inaendana na thamani ya fedha iliyotumika.
Ikumbuke kuwa halmashauri ya Arusha ilipokea jumla ya shilingi milioni 110 kwa ajili ya ujenzi wa vituo vitano vya walimu, huku kila kituo kikigharimu shilingi milioni 22, zikijumuisha ujenzi wa baadhi ya vituo na ununuzi wa samani za kituo.
ARUSHA DC ni Yetu, Tushirikiane Kuijenga"
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.