Wajumbe wa Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango halmashauri ya Arusha, wametembelea na kukagua utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Kituo kipya cha Afya cha Matevesi, kata ya Mateves, fedha kutoka Mapato ya Ndani ya Halmashauri ya Arusha.
Wajumbe hao wa kamati ya Fedha, wameridhishwa na utekelezaji wa mradi huo, kwa kuwataka watalamu kwa kushirikiana na kamati ya ujenzi, kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati, kwa kuzingatia ubora wa majengo unaolingana na thamani ya fedha.
Akizungumza wakati akiwawasilisha taarifa ya utekelezaji wa ujenzi huo, Afisa Mtendaji wa Kata ya Mateves Muyai Kivuyo, ameweka wazi kuwa, halmashauri kupitia mapato yake ya Ndani inategemea kutekeleza mradi huo wa ujenzi wa kituo kioya cha Afya, kwa ghrama ya shilingi milioni 197, kwa hatua tofauti.
Ameongeza kuwa mpaka sasa, halmashauri imetoa shilingi milioni 69 za kuanza ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje ( OPD), ujenzi ambao uko katika hatua ya ujenzi wa msingi na jamvi, tayari kwa kuanza kupandisha boma la jengo hilo.
Hata hivyo KaimuAfisa Mipango Albert Mahoo, amebainisha kuwa, ujenzi wa kituo hicho cha Afya, unategemea kukamilika, mwishoni mwa mwaka huu wa fedha, mwezi Julai 2022, huku halmashauri ikitoa fedha hizo kwa awamu kadri mapato ya ndani yanavyopatikana.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.