Na Elinipa Lupembe
Kamati ya Fedha Utawala na Mipango, halmashauri ya Arusha, wakikagua mradi wa ujenzi wa nyumba ya mtumishi Kituo cha Afya Nduruma, kata ya Nduruma.
Mradi huo wa nyumba ya mtumishi uko katika hatua za mwisho za ukamilishaji na umegharimu kiasi cha shilingi milioni 50 fedha kutoka Serikali Kuu, ikiwa ni utekelezaji wa malengo ya Serikali ya kuboresha na kurahisisha upatikanaji wa huduma za afya nchini.
Wajumbe hao wamemtaka Mkurugenzi wa halmashauri kuhakikisha fundi anafanya marekebisho madogo madogo yaliyosalia, na kuwataka kuweka matanki ya kuvunia maji ili kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa maji safi na taka katika maeneo mengi.
Hata hivyo, Mkuu wa Idara ya Ujenzi Mhandisi Nuru Mkwazu, amepokea maoni hayo na kufafanua kuwa, idara imejipanga kuhakikisha majengo hayo yanakuwa na miundo mbinu ya kuvunia maji katika majengo yote kwenye Taasisi za Umma.
Ziara hiyo ya kikazi ya kamati ya Fedha, Utawala na Mipango ni ya kawaida kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za uendeshaji wa serikali za Mitaa kwa kuzingatia Utawala Bora wa uwazi na uwajibikaji.
RUSHA DC
KaziIendelee✍✍
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.