Wajumbe wa Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango, wametembelea na kukagua mradi wa Kikundi cha Vijana cha KIDALI YOUTH GROUP kilichopo kata ya Mwandet, kukundi kilichopewa mkopo usio na riba kiasi cha shilingi milioni 10 ikiwa ni asilimia 10 za mapato ya ndani ya halmashauri.
Akisoma taarifa ya maendeleo ya mradi huo, Katibu wa Kikundi, Elibariki Mollel, amesema hadi sana mradi umefikia mtaji wa milioni 12.3 kutoka wa milioni 2.3 waliokuwa nao hapo awali kabla ya kupata mkopo.
Amefafanua kuwa baada ya kupokea mkopo wa shilingi milioni 10 kutokaka halmshauri walifanikiwa kununua ng'ombe pamoja na kondoo, ambao wanawanenepesha na kuwauza tena kwaajili ya kijipatia faida na kukuza mradi.
"Tunaishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuendelea kutoa fursa kwa vijana wanawake na walemavu kupitia mikopo isiyo na riba inayotolewa na halmashauri zote nchini na kuwahimiza vijana wenzao kuacha kulalamika badala yake kufanya kazi kulingana na mazingira wanayoishi".Alisema katibu huyo
Naye Diwani Viti Maalum CCM, Mhe. Grace Seneu ameonyesha kufurahishwa na mradi huo wa kikundi cha vijana wakiwa na maendeleo mazuri, na kuwataka watalamu wa halmashauri kuendelea kuwasimamia ili wapige hatua zaidi ili vijana wengine waweze kuiga mfano huo.
Naye Afisa Maendeleo ya Jamii, Halmashauri ya Arusha Stedvant Kileo, ameahidi kusimamia kikundi hicho katika hatua zote kwa kutoa ushauri wa mradi na utunzaji wa fedha mpaka hapo watakapoweza kusimama kibiashara.
ARUSHA DC ni Yetu, Tushirikiane Kuijenga"
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.