Wajumbe wa Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango, wametembeleana kukagua mradi wa ujenzi wa uzio shule ya Msingi Ilboru ambao umejengwa kwa ajili ya usalama wa wanafunzi wenye mahitaji maalum.
Akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi huo, Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi, Mwl. Philomena Mbilinyi, amesema kuwa ujenzi wa ukuta wenye urefu wa Mita 386, umetekelezwa kwa gharama ya shilingi milioni 50 fedha kutoka Serikali Kuu, ujenzi, ambao tayari umekamilika kwa asilimia 90.
Ameongeza kuwa uwepo wa uzio shuleni hapo, umeongeza usalama wa wanafunzi hasa wenye mahitaji maalumu wanaolala shuleni hapo, pamoja na usalama wa mali za shule na kuzuia watoto kutoroka kwa wanafunzi wakati wa vipindi hali inayopelekea ufaulu wa wanafunzi hao kuongezeka.
Hata hivyo wajumbe hao wa kamati ya fedha, wamepongeza utekelezaji wa mradi huo, ambao una manufaa makubwa kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum hasa walemavu wa ngozi.
ARUSHA DC ni Yetu, Tushirikiane Kuijenga"
ARUSHA DC
KaziInaendelea✍✍
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.